Maandalizi ya mchezo namba 218 wa ligi kuu ya soka Tanzania bara kati ya Mbeya City fc na Yanga ya Dar es Salaam uliopagwa kuchezwa kesho kwenye uwanja wa Sokoine jijini hapa yamekamilika na kinachosubiriwa ni dakika 90 hapo kesho.
Kwa mujibu wa msimamizi wa kituo cha Mbeya ambaye pia ni katibu mkuu wa chama cha soka mkoa, Haroub Suleiman, mchezo huo utafanyika kama ulivyopangwa kwa sababu timu zote mbili tayari zisharipoti (kuwepo) kituoni na tayari makubaliano juu ya kiingilia yashafikiwa.
“Yanga wamewasili asubuhi ya leo, hii ina maana kuwa mchezo upo kama ulivyopangwa, kutokana na uzito wa mchezo wenyewe,tumekubaliana kiingilio kitakuwa shilingi 5000, nawaomba mashabiki wote wa soka katika kanda hii ya nyanda za juu kusini wajitokeze kwa wingi kuzishangilia timu zao huku pia wakitakiwa kudumisha amani kabla na baada ya mchezo” alisema.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Mbeya City Fc, Mussa Mapunda amewatakia kila la kheri na kuwashukuru mashabiki wote wa timu yake popote walipo ndani na nje ya nchi kwa jinsi walivyojitolea kuisapoti timu yao tangu ilipopanda daraja na kuwataka kujitokeza kwa wingi hapo kesho kuja kuisapoti na kushuhudia City ikiandikisha ushindi wa kwanza mbeya ya Yanga.
No comments:
Post a Comment