Wednesday, 30 March 2016

WADAU WA SEKTA YA USAFIRI WA ANGA WAKUTANA KUJADILI USAFIRI WA ANGA (CIVIL ATIVIATION MASTER PLAN) DAR ES SAALAM.

10
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi  na Mawasiliano, Dkt Leonard Chamuriho(katikati) Mkurugenzi Mkuu wa TCAA, Hamza Johari(Kulia)  na Kaimu Mkurugenzi Mkuu  wa Mamlaka

UFAFANUZI KUHUSU KIMA CHA CHINI KUHUSU MAFAO YA WASTAAFU PITIA HAPA.

index

TAARIFA KWA UMMA
Hivi karibuni Mamlaka imekuwa ikipokea Malalamiko mengi kutoka kwa wanachama na wadau mbalimbali

WALIOKATA TIKETI KWAAJILI YA PAMBANO KATI YA STARS NA CHAD KURUDISHIWA FEDHA ZAO.

b
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetangaza kuwarudishia fedha zao kesho Jumanne, wapenzi wa mpira wa miguu waliokuwa wameshakata tiketi za kushuhudia mchezo wa kundi G kati ya Tanzania v Chad jijini Dar es salaam.

AZAMU YANGA WAINGIA WOTE DIMBANI ALHAMISI KUWAKABILI WAHASIMU WAO.

asfclounge
Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup) linatarajiwa kuendelea Alhamisi kwa michezo miwili kuchezwa katika hatua ya robo fainali ya michuano hiyo.

PROF.MBARAWA AFANYA ZIARA YAKUSHTUKIZA KOJ KURASINI HABARI ZAIDA HAPA.

1
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akiongea na baadhi ya wafanyakazi wa TPA eneo la kupakulia mafuta yanayoingia nchini (KOJ) Kurasini

SERSNGETI BOYS YAELEKEA KUMINYANA NA MISRI.

serengeti-new
Timu ya Taifa ya Vijana wenye umri chini ya miaka 17 (Serengeti Boys) inatarajiwa kucheza michezo miwili ya kirafiki na timu ya Taifa ya Misri Vijana wenye umri chini ya miaka 17 (The Pharaohs) jijini Dar es salaam.
Mchezo wa kwanza kati ya Serengeti Boys dhidi ya The Pharaohs utachezwa siku ya Jumamosi, Aprili 2 katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, huku mchezo wa pili ukichezwa Jumanne Aprili 5 katika uwanja wa Azam Complex Chamazi.
Msafara wa The Pharaohs unatarajiwa kuwasili Alhamis tarehe 31, Machi ukiwa na watu 33, wakiwemo wachezaji 25 pamoja na viongozi 8, na wataondoka nchini tarehe 6 Aprili kurudi kwao nchini Misri.
Kikosi cha Serengeti Boys kinachonolewa na makocha Bakari Shime na Sebastian Mkomwa wakishauriwa na Jan Poulsen, kimeendelea na mazoezi katika uwanja wa Karume, zilipo ofisi za Makao za Makuu ya TFF.
Serengeti Boys ilingia kambini takribani wiki mbili zilizopita katika hosteli za TFF zilizopo Karume, kujiandaa na michezo hiyo miwili ya kirafiki ya kujipima nguvu kujiandaa kuwania kufuzu kwa Fainali za Mataifa ya Afrika kwa Vijana wenye umri chini ya miaka 17 zitakazofanyika mwaka 2017 nchini Madagascar.
Tanzania itaanza kuwania kufuzu kwa fainali hizo mwishoni mwa mwezi Juni, kwa kucheza dhidi ya timu ya Taifa ya Vijana ya Shelisheli.


Kanye West asema huu ndio wimbo wake bora wa mwaka 2015.

Rapa Kanye West ametumia instagram yake kutufahamisha kuwa

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA MAENDELEO YA MIUNDO MBINU YAFANYA ZIARA YATEMBELEA MRADI WA UPANUZI WA UWANJA WA NDEGE.YA

 KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Maendeleo ya Miundombinu, imefanya ziara ya kutembelea mradi wa upanuzi wa uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (Terminal Three- TBIII), jijini Dar es Salaam, Machi 29, 2016 ambapo awali wajumbe wa kamati hiyo inayoongozwa na Profesa Norman Adamson Sigalla King, walipatiwa maelezo ya kina ya maendeleo ya mradi huo unaohusisha jengo la kisasa la abiria na sehemu ya kuegesha ndege kwa ajili ya kupakia na kushusha abiria na sehemu ya maegesho ya magari. Baada ya maelezo hayo ya kina yaliyotolewa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Nchini, (TAA), Mhandisi George Sambali akisaidiana na baadhi ya wakurugenzi wengine wa Mamlaka hiyo, wajumbe hao walitembelea mradi huo na kujionea hatua mbalimbali za ujenzi ambapo kwa sasa ujenzi umefikia karibu asilimia 60. Pichani, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TAA, Mhandisi George Sambali, (kushoto), akitoa maelezo kwa Mwenyekiti wa Kamati hiyo ya Bunge, Norman Adamson Sigalla King, (kulia), na baadhi ya wajumbe na maafisa wa TAA

IZZO BISSNESS ALIUVYO WAPAGAWISHA WAKAZI WA JIJI LA MBEYA NA VIUNGA VYAKE SOMA HAPA..



Mamia ya mashabiki wakifurahia burudani toka kwa Izzo  Bizness

SERIKALI YAJIPANGA KUWASIDIA WAKULIMA ILI KUPAMABANA NA MABADILIKO YA TABIA YA NCHI NA HALI YA HEWA.

DSC_1667
Wageni rasmi katika mkutano huo, Wa kwanza kushoto ni Mtafiti kutoka Taasisi ya Mtandao wa Kutathimini Sera za Chakula, Kilimo na Maliasili (FANRPAN), Njongenhle Nyoni, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF), Dkt. Tausi Kida na Mkuu wa Kitengo cha Mazingira kutoka Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Bi. Shakwaanande Natai

.
Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi imejipanga kuhakikisha inawasaidia wakulima kupambana na mabadiliko ya tabia ya nchi ambayo yanaonekana kuendelea kuikabili nchi.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Kitengo cha Mazingira kutoka Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Bi. Shakwaanande Natai alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano ulioandaliwa na Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF) na Taasisi ya Mtandao wa Kutathimini Sera za Chakula, Kilimo na Maliasili (FANRPAN) ili kujadili mpango wa Kilimo Salama (CSA).
Bi. Natai alisema serikali inatambua uwepo wa mabadiliko ya Tabia ya Nchi na kwasasa tayari wataalamu wanafanya tafiti ili waone ni jinsi gani wanaweza kuwasaidia wakulima kupambana na mabadiliko hayo.
Alisema kwa sasa bado wakulima wengi hawajafahamu kama kuna mabadiliko ya tabia ya nchi na hivyo wamekuwa wakitumia njia za asili lakini baada ya utafiti watapatiwa mbinu mpya za kupambana na mabadiliko ambapo wataweza kutumia njia za kisasa ambazo zinaonekana kuwa bora zaidi.
“Serikali inatambua na tunajipanga kuwasaidia wakulima, shida kwa sasa bado wakulima wengi hawajajua kama kuna mabadiliko ya tabia ya nchi lakini wataalamu wapo wanafanya tafiti baada ya hapo tutajua tunawasaidia vipi,
“Kwa sasa kinachoonekana ni kutokueleweka kwa hali ya hewa kama mafuriko kutokea lakini kwa kuwa bado hawajapatiwa elimu wanashindwa kutambua na bado wanatumia njia za asili, tutawapa mbinu mpya watafanya kwa pamoja na mbinu wanazotumia sasa za asili,” alisema Bi. Natai.
Aidha alieleza kuwa baadhi ya huduma ambazo watapatiwa wakulima baada ya kukamilika kwa tafiti ni pamoja na kupewa elimu ya kilimo cha umwagiliaji, mbegu za kisasa ambazo zinawahi kukomaa na dawa za kupambana na magonjwa.
Nae mtafiti kutoka FANRPAN, Njongenhle Nyoni alisema taasisi yake imefanya mkutano huo ili kuona ni jinsi gani wanaweza kupambana na mabadiliko ya tabia ya nchi katika nchi ambazo wanafanya kazi ambapo Tanzania ni mojawapo.
Alisema wao wanafanya tafiti kuona hali ilivyo na baada ya hapo wanatazama changamoto zilizopo katika kupambana na mabadiliko na wanatoa ushauri ni jambo gani linaweza kufanyika ili kuwezesha kufanikisha kufanyika Kilimo Salama (CSA).
“Tunakutana na watu kutoka asasi za kijamii na taasisi mbalimbali ili kuona ni jinsi gani CSA inaweza kufanya kazi vizuri hasa katika maeneo tunafanya nao kazi na hii sio Tanzania tu hata mataifa mengine kama Malawi tunalifanya hili,” alisema Nyoni.
Pia iliongeza kuwa malengo ya FANRPAN ni kusaidia wakulima kuondoka katika janga la umasikini lakini pia kuwepo kwa chakula kilicho katika hali ya usalama bila kuathiriwa na mabadiliko ya tabia ya nchi.
DSC_1671
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF), Dkt. Tausi Kida akitoa neno la ufunguzi.

UBALOZI NCHINI INDIA WAADHIMISHA ITEC DAY SOMA HAPA.

3
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora  Mh. Angellah Kairuki (Mb) akizungumza katika maadhimisho ya  Siku ya Ushirikiano wa Kiufundi  na Kiuchumi  kati ya Tanzania na India (ITEC DAY) yaliyofanyika katika Kituo cha Utamaduni cha  India jijini  Dar es Salaam.

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI AFANYA ZIARA KIGOMA.

KIS1
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati), akisalimiana na wafanyakazi wa Mashirika mbalimbali ya Kitaifa na Kimataifa yanayohudumia wakimbizi katika Kambi ya muda ya NMC, iliyoko mkoani Kigoma, kushoto ni Mratibu wa Wakimbizi  Mkoani  Kigoma, Tonny  Samwel  Laiser.Naibu Waziri yupo mkoani Kigoma kwa ziara ya kikazi.


KIS2
Msimamizi  wa  Kambi ya muda ya NMC, Jordan Emmanuel (wa kwanza kushoto), akimuonyesha Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, jinsi mfumo wa jiko la kupikia chakula  kambini hapo unavyofanya kazi.Naibu Waziri yupo mkoani Kigoma kwa ziara ya kikazi.

KIS3
Sehemu ya vitanda vipya vikiwa katika moja ya mabweni ya Kambi ya muda ya wakimbizi ya NMC , tayari kwa kufungwa na kuanza kutumika na wakimbizi wanaohifadhiwa kambini hapo.