Sunday, 1 May 2016
WAZIRI MHAGAMA ATOA TAARIFA YA HALI YA DAWA ZA KULEVYA NCHINI YA MWAKA 2014.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Bunge, Mhe Jenista Mhagama (kushoto) akitoa taarifa kwa waandishi wa habari mwishoni mwa wiki mjini Dodoma kuhusu hali ya dawa za kulevya nchini ya mwaka 2014 na jinsi dawa hizo zinavyoathiri afya na nguvu kazi ya taifa. Kulia ni Mfamasia Sehemu Elimu, Habari na Takwimu Tume ya Kuratibu Udhibiti wa Dawa za kulevya nchini Amani Masami.
Picha,Dj Khaled athibitisha kiki lake kwenye ziara ya Beyonce,wasanii watumia fursa kupiga picha na JayZ.
Baada ya wadau kuchukulia powa uwezo wa Dj Khaled kwenye ziara za Beyonce Dj huyu maarfu kwa kuwaleta wasanii pamoja kwenye colabo kali amemtupia rapa Li Wayne, Future na Rick Ross kwenye stage moja mjini Miami kwenye show yake iliyokalisha zaidi.
Itazame hapa video mpya ya rapa K.O wa Afrika kusini ‘Papa Action’ Enjoy.
South African rapper, Ntokozo Mdluli aka K.O aliyewahi kuwa na kundi la Teargas, ametoa video mpya ya wimbo wake wa “Papa Action“, sehemu kubwa ya hii video imefanyika nchini Marekani.
Bonyeza Play Kuitazama.
Picha,Ata baada ya tetesi za usaliti, bado Beyonce na Jay Z wanacheka pamoja.
Hivi karibuni pamekuwa na stori kibao kuhusu usaliti uliofanywa na Jay Z na mwanamke ambaye ametajwa kwa jina la husika wa BECKY tu kwenye wimbo wa ‘Sorry’ wa Beyonce.
Utata wa wimbo wa Sugu na Mr Blue wamalizwa Friday nite live,stori imewekwa hapa kama ulipitwa.
Hatua hiyo imekuja baada ya kuwepo kwa malalamiko kutoka kwa msanii Mr Blue aliyekuwa akidai kuwa Sugu amebadilisha ngoma yake aliyokuwa amemshirikisha, na kuondoa mashairi yake bila ya ruhusa yake, na kasha kuitoa kwenye media.
Master j asema maproducer wa muziki Bongo wana hali mbaya sana.
Mtayarishaji mkongwe wa muziki Tanzania, Master J ambaye pia ni mmiliki wa lebel ya Mj Records inayoendeshwa na Marco Chali ameongelea hali mbaya ya maproducer wa Tanzania kwa sasa.
Master J akiongea kwenye kipindi cha FNL, alisema “Maproducer wa muziki Bongo wanahalimbaya sana, madirector ndiyo wanamiliki magari na majumba,kama inawezekana wasanii waende kufanya show mikoani na video zao halafu waone itakuwaje,”
WAFANYAKAZI WA MFUKO WA PENSHENI WA PPF WASHIRIKI SHEREHE ZA MEI MOSI MKOA WA DAR ES SALAAM.
Baadhi ya Wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni PPF, wakiwa katika maandamano wakipita mbele ya mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (hayupo pichani) wakati wa sherehe za maadhimisho ya siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi) zilizofanyika kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, leo.
MFUKO WA FIDIA KWA WAFANYAKAZI, WCF, WASHIRIKI SHEREHE ZA MEI MOSI KWA MARA YA KWANZA
Baadhi ya wafanyakazi wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, WCF, wakishiriki matembezi yakilele cha siku ya Wafanyakazi Duniani (May day), hapa matembezi yakiwa barabara ya Nyerere jijini Dar es Salaam, Mei 1, 2016.
NA K-VIS MEDIA/Khalfan Said
SWANSEA YAICHAKAZA LIVERPOOL NA KUJIOKOA KUSHUKA DARAJA.
VYAMA VYA SIASA VIMEKUTANA KUJADILI MAPENDEKEZO YA MFUMO WA UTATUZI WA MIGOGORO NDANI NA BAINA YA VYAMA.
Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa Nchini Mhe. Peter Kuga Mziray akifafanua jambo wakati wa kikao cha Baraza kujadili Mapendekezo ya Mfumo wa utatuzi wa migogoro ndani na baina ya vyama vya siasa kilichofanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa GEPF Victoria Jijini Dar es salaam . Kulia ni Mhe. Jaji Francis S.K Mutungi, Msajili wa Vyama vya Siasa na Mhe. Vuai Ali Vuai, Makamu Mwenyekiti wa Baraza .
WAHALIFU WAWEKEWA MKAKATI MZITO DODOMA.
Katika kuhakikisha wahalifu hawapati nafasi ya kutamba nchini, makamanda wa Polisi wa mikoa, wakuu wa upelelezi na waendesha mashtaka wameazimia kuboresha ushirikiano wao katika kufanikisha kesi za wahalifu pindi zinapofikishwa mahakamani ili waweze kupewa adhabu kali kwa mujibu wa sheria.
DK. SHEIN AONGOZA SIKU YA KILELE CHA SIKUKUU YA WAFANYAKAZI ZANZIBAR
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akipokea maandamano ya Wafanyakazi mbali mbali wa Taasisi za Serikali na Binafsi, wakipita mbele yake wakati wa sherehe za siku ya Wafanyakazi Duniani katika viwanja vya Ukumbi wa Salama Bwawani Mjini Unguja leo,[Picha na Ikulu.]
Subscribe to:
Posts (Atom)