Msajili wa Vyama vya Siasa nchini Mhe. Jaji francis S. K Mutungi pamoja
na Maaafisa Wandamizi kutoka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa wakiwa
nje ya ukumbi wa Saadan wa Mwalimu Nyerere Jijini Dar es salaam Leo
kabla ya kuanza kikao cha kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria
cha kupitisha bajeti ya mwaka 2016/2017 ya Ofisi ya Msajili wa Vyama vya
Siasa.
Waziri
wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama
akijibu hoja za wajumbe kwenye kikao cha kamati ya Kudumu ya Bunge ya
Katiba na Sheria cha kupitisha bajeti ya Ofisi ya Msajili wa Vyama vya
Siasa kilichofanyika Leo katika ukumbi wa Saadan wa Mwalimu Nyerere
Jijini dar es salaam.
Mhe.
Dkt Abdallah Possi, Naibu Waziri (Ofisi ya Waziri Mkuu) Sera, Bunge,
Kazi , Vijana, Ajira na Ulemavu akiteta jambo na Msajili wa vyama vya
Siasa Mhe. Jaji Francis S.K Mutungi kwenye kikao cha kamati ya Kudumu
ya Bunge ya Katiba na Sheria cha kupitisha bajeti ya mwaka 2016/2017 ya
Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kilichofanyika Leo katika ukumbi
wa Saadan wa Mwalimu Nyerere Jijini dar es salaam.
Msajili
wa Vyama vya Siasa Nchini Mhe. Jaji Francis S.K Mutungi akitoa
ufafanuzi wa hoja za wajumbe kwenye kikao cha kamati ya Kudumu ya Bunge
ya Katiba na Sheria cha kupitisha bajeti yam waka 2016/2017 ya Ofisi ya
Msajili wa Vyama vya Siasa kilichofanyika Leo katika ukumbi wa Saadan
wa Mwalimu Nyerere Jijini dar es salaam. Kushoto ni Waziri wa Sera,
Bunge, Kazi , Vijana, Ajira na Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama na Manaibu
waziri ,Mhe Antony P. Mavunde na Mhe. Dkt Abdallah Possi
Mjumbe
wa kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria, Mhe Richard Ndassa
akiwasilisha hoja kwenye kikao cha kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba
na Sheria cha kupitisha bajeti ya mwaka 2016/2017 ya Ofisi ya Msajili
wa Vyama vya Siasa kilichofanyika Leo katika ukumbi wa Saadan wa
Mwalimu Nyerere Jijini dar es salaam. Kulia ni wajumbe wa kamati.
Waziri
wa Sera, Bunge, Kazi , Vijana, Ajira na Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama
akijibu hoja za wajumbe kwenye kikao cha kamati ya Kudumu ya Bunge ya
Katiba na Sheria cha kupitisha bajeti ya Ofisi ya Msajili wa Vyama vya
Siasa kilichofanyika Leo katika ukumbi wa Saadan wa Mwalimu Nyerere
Jijini dar es salaam. Kulia ni Mhe. Dkt Abdallah Possi, Naibu waziri wa
Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu .
Angelina
Sanga, Katibu kiongozi wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria
akiwapitisha wajumbe (hawapo pichani) kwenye vifungu vya bajeti ya
mwaka 2016/2017 ya Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kwenye kikao cha
kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria cha kupitisha bajeti ya
Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kilichofanyika Leo katika ukumbi wa
Saadan wa Mwalimu Nyerere Jijini dar es salaam.
Waadhi
ya wajumbe wa kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria
wakifuatilia kwa makini mawasilisho ya bajeti ya mwaka 2016/2017 ya
Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kwenye kikao cha kamati ya Kudumu ya
Bunge ya Katiba na Sheria cha kupitisha bajeti ya Ofisi ya Msajili wa
Vyama vya Siasa kilichofanyika Leo katika ukumbi wa Saadan wa Mwalimu
Nyerere Jijini dar es salaam.
Wajumbe
wa Kamati ya Kudumu ya Bunge na Sheria wamepewa rai ya kushikamana na
Serikali katika kuhakikisha kuwa maboresho ya Sheria ya Vyama vya Siasa
ya mwaka1992 na Sheria ya gharama za uchaguzi ya mwaka 2010 yanafanyika
ili kuondoa utata na migongano ya utekelezaji wa masuala ya siasa
nchini.
Hayo
yamesemwa na Waziri wa Sera, Bunge, Kazi , Vijana, Ajira na Ulemavu
Mhe. Jenista Mhagama wakati akijibu swali kutoka kwa wajumbe kwenye
kikao cha kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria cha kupitisha
bajeti ya Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kilichofanyika Leo katika
ukumbi wa Saadan wa Mwalimu Nyerere Jijini dar es salaam ambao walihoji
uhalisia wa utekelezaji wa sheria zililizopo sasa.
Wajumbe
hao walihoji utitiri wa vyama vingi nchini ambavyo miaka nenda rudi
havina madiwani wala wabunge na vingine kutoshiriki katika chaguzi .
Wajumbe pia walihoji gharama ndogo za usajili wa vyama vya siasa
ukilinganisha na hali ya maisha iliyopo kwa sasa.
Jambo
lingine ambalo wajumbe wamehoji ni nafasi ya Msajili wa Vyama vya Siasa
katika kushughulikia migogoro ya kisiasa ndani na nje ya Vyama vya
Siasa na ushirikishwaji wa wanawake katika maamuzi ndani ya vyama vya
siasa.
Akijibu
hoja hizo Mhe Mhagama amesisitiza kuwa maboresho ya Sheria ya Vyama vya
Siasa na Sheria ya Gharama za uchaguzi ndio njia pekee itakayompa meno
Msajili wa Vyama vya Siasa nchini katika kutekeleza majukumu yake
ipasavyo.
“Sheria
tulizonayo ndio inatoa mwanya wa haya yote haya na ndio maana Serikali
kwa sasa inaendelea na taratibu za kuboresha sheria hizi, tayari Ofisi
ya Msajili wa Vyama vya siasa ameshawasilisha mapendekezo ya maboresho
ya Sheria ya Vyama vya Sasa na Sheria ya gharama za uchaguzi na sisi
tumeridhia , tunasubiri tu bunge kujadili ili ziweze
kutumika”alisisitiza mhe Mhagama