Thursday, 7 April 2016

Winnie mandela agoma madai ya kumiliki nyumba.

Mtalaka wa Mzee Nelson Mandela, Winnie Mandela amejikuta akigonga mwamba mahakamani baada ya shauri lake alilofungua la madai ya kupewa umiliki wa nyumba ya Mandela iliyopo Kijiji cha Qunu, kutupiliwa mbali.

UMOJA WA ULAYA(EU) WAZINDUA PROGRAMU WA KUZISAIDIA ASASI ZISIZO ZA KISERIKALI HAPA NCHINI

Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania, Bw. Roeland Van De Geer kizungumza jambo wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa programu ya kusaidia mashirika yasiyo ya kiserikali iliyofanyika jana. Picha na Geofrey Adroph

Je ulipitwa na story ya Rais Magufuli na Rais Kagame Kigali leo kwenye kumbukumbu ya mauaji ya Kimbari .


Rais John Pombe Magufuli wa Tanzania yupo nchini Rwanda kwenye ziara ambayo ameianza

Je unajua vitu vingi vya ajabu vyatokea dunia Mwanafunzi wa kiume apata ''hedhi''

George Fellowes ni mwanafunzi wa chuo kikuu mwenye umri wa miaka 22 na anaamni kwamba hata yeye hupatwa na ''hedhi ya kiume''.

HUU NDIO MSIMAMO WA UFARANSA WAPITISHA SHERIA INAYOKATAZA KUNUNUA NGONO.

Nchi ya Ufaransa imepitisha sheria inayokataza kulipia ngono na mtu atakayebainika kutenda kosa la kununua ngono atatozwa faini ya dola 4,274.

Unajua nini kimempata Kapombe kuwakosa Esperance Beki wa Azam



Beki wa Azam FC, Shomary Kapombe hatacheza mechi zote mbili za Kombe la Shirikisho la Soka Afrika (CAF) dhidi ya Esperance ya Tunisia.
Beki wa Azam FC, Shomary Kapombe hatacheza mechi zote mbili za Kombe la Shirikisho la Soka Afrika (CAF) dhidi ya Esperance ya Tunisia.

Kapombe aliyekosa mechi mbili mfululizo za Ligi Kuu timu hiyo ikitoa sare zote, 1-1 na Toto mjini Mwanza Jumapili na 2-2 na Ndanda hapo jana, anatarajiwa kusafirishwa kwenda Afrika Kusini kwa matibabu.


Daktari wa Azam FC, Juma Kwimbe amesema kwamba Kapombe hatacheza mechi zote dhidi ya Esperance Jumapili Dar es Salaam na wiki mbili zijazo Tunis kwa sababu ni mgonjwa.
.

Je wajua neno la mwisho alilolisema Haji manara juu ya TFF.

Haji Manara-Afisa habari Simba SC

Mkuu wa kitengo cha habari wa klabu ya Simba SC, Hajji Manara ameiomba Taasisi ya Kupambana na Kuzia Rushwa nchini-TAKUKURU kuweka kambi na kufanya uchunguzi yakinifu katika Shirikisho la soka nchini, TFF ambalo limegubikwa na tuhuma za rushwa na upangaji matokeo katika michezo miwili ya mwisho katika ligi daraja la kwanza.

Haya ndio yaliyo ajili sudani kusini Riek Machar kurudi Juba kwa wadhfa mpya.


 Riek Machar

Kiongozi wa upinzani nchini Sudan Kusini Riek Machar amethibitisha kwamba atarudi katika mji mkuu wa taifa hilo Juba mnamo mwezi Aprili tarehe 18.

Je wajua Wateja wa Chase Bank waingiwa na wasiwasi Kenya story nzima iapo hapa.


 Wateja wengi wamefika katika matawi ya benki hiyo wakitaka kutoa pesa zao

Benki moja nchini Kenya imewekwa chini ya mrasimu baada ya wateja kutoa pesa zao kwa wingi kufuatia wasiwasi kuhusu uthabiti wa benki hiyo.
Wengi wa wateja wamefika kwa wingi katika mashine za kutolea fedha (ATM) leo lakini wakapata mashine hizo zimefungwa.

Benki Kuu ya Kenya (CBK), taasisi iliyo na jukumu la kusimamia huduma za benki Kenya, imeamua kuweka benki hiyo ya Chase Bank chini ya mrasimu ikisema benki hiyo ilishindwa "kutimiza masharti yake kifedha tarehe 6 Aprili”.

CBK imesema hatua hiyo imechukuliwa kwa maslahi ya „walioweka pesa kwenye benki hiyo, wanaoidai pesa benki hiyo na umma.”

Benki hiyo sasa itasimamiwa na shirika la Kenya Deposit Insurance Corporation (KDIC).

Gavana wa CBK Dkt Patrick Njoroge ameambia wanahabari kwamba Chase Bank haikuweza kutimiza mahitaji ya kimsingi kama vile „kuhamisha pesa za wateja”.

Matawi yote 62 ya benki hiyo nchini Kenya yalifungwa jioni, Dkt Njoroge akisema hatua hiyo ilitumiwa kuilinda benki hiyo baada ya wateja wengi kujitokeza kutoa pesa.


                                                                                                                                                                                                         Jumatano, Chase Bank ilitangaza kwamba mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi Zafrullah Khan na mkurugenzi mkuu Duncan Kabui walikuwa wamejizulu baada ya kuchapishwa kwa taarifa ya matokeo ya kifedha ya mwaka 2015.
Benki hiyo ilimteua Muthoni Kuria kuwa mwenyekiti wa bodi hiyo na kuwahakikishia wateja wake kamba benki hiyo iliyohudumu kwa miaka 20 nchini Kenya ilikuwa imara.

Nape akiri udhaifu Sheria ya Magazeti Waziri wa habari atikisa kwa hili.


Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye  

Kigoma. Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye amekiri kwamba Sheria ya Magazeti ya Mwaka 1976, aliyoitumia kulifuta Gazeti la Mawio ni mbaya inahitaji kufanyiwa marekebisho.

Je unajua nini kimeendelea katika mahakama ya rufani kusikiliza mashauri 400 dodoma ipo hapa.

Dodoma. Mahakama ya Rufani itasikiliza rufaa 40 na kutoa hukumu katika vikao vyake vinavyoendelea mjini Dodoma.