Monday, 11 April 2016

Kanzidata ya Watu Wenye Ulemavu yazinduliwa


POZ1
Naibu Waziri Ofisi ya Wazikri Mkuu (watu wenye Ulemavu) Mhe. Dkt. Abdallah Possi akifafanua jambo wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Kanzidata ya watu wenye ulemavu katika Ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu Aprili 11, 2016

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AKUTANA NA BALOZI WA IRAN HAPA NCHINI. AKABIDHIWA CHETI NA WATU WENYE ULEMAVU


MAKA1
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Balozi wa Iran Nchini Tanzania Mhe. Mehd Aghajafari wakati Balozi huyo alipofika Ofisini kwa Makamu wa Rais Ikulu Dar es salaam leo April 11,2016, kwenye mazungumzo yao Viongozi hao wamezungumzia suala la kukuza Ushirikiano kati ya Nchi mbili hizi.

WANAWAKE WAFANYABIASHARA MASOKONI WATAKIWA KUWA CHACHU YA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA KATIKA MAENEO YAO YA BIASHARA


 Mwenyekiti wa Soko la Kisutu Tamimu Chande akizungumza katika Kampeni ya Kuongeza uelewa wa kupinga ukatili wa Kijinsia katika Soko la Kisutu Dar es Salaam leo asubuhi. Kampeni hiyo inaendeshwa na Shirika la Eqiuality for Growth (EfG).

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu azindua taasisi ya (Basila Mwanukuzi Empowerment Foundation)Waziri wa Afya Ummy Mwalimu azindua taasisi ya (Basila Mwanukuzi Empowerment Foundation)


1
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy

MFUNGWA AUSTRALIA AMCHONGA NYWELE MWENZAKE KAULIMBIU YA KUNDI LA IS.

Mfungwa mmoja mwenye umri wa miaka 18 nchini Australia anayeliunga mkono kundi la la Dola ya Kiislam, amedaiwa kutumia kisu kumchonga kichwani mfungwa mwenzake kaulimbiu ya kundi hilo.

Taarifa zinasema mfungwa huyo alimchonga nywele kichwani mfungwa mwenzake maandishi e4e, ikiwa ni kifupi cha maneno eye for an eye, ambayo kwa lugha ya Kiswahili yanaamana ya Jicho kwa Jicho.

Uchunguzi umeshaanzishwa kubaini ni kwa jinsi gani kijana huyo hatari aliweza kuwekwa pamoja na mfungwa mwenzake mwenye umri wa miaka 40.

RAIS DK. MAGUFULI AAGIZA BILIONI 6 KUTOKA BUNGE ZIKABIDHIWE KWA MAGEREZA NA JKT ILI KUTENGENEZA MADAWATI 120.000RAIS DK. MAGUFULI AAGIZA BILIONI 6 KUTOKA BUNGE ZIKABIDHIWE KWA MAGEREZA NA JKT ILI KUTENGENEZA MADAWATI 120.000


MLO3
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Hundi Kifani yenye thamani ya Shilingi Bilioni Sita kutoka kwa Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson mara baada ya Taasisi ya Bunge kutekeleza kwa vitendo kauli ya kubana matumizi yasio na Tija ili fedha hizo zikanunulie madawati kwa ajili ya wanafunzi.

Rais Magufuli ameipongeza ofisi ya Bunge kwa kubana matumizi na kufanikiwa kuokoa shilingi Bilioni 6, ambazo zitatumika kutengeneza madawati ya wanafunzi wa shule na amezitaka ofisi na taasisi nyingine za serikali kuiga mfano huo.
Ameagiza fedha hizo zipelekwe Idara ya Magereza na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) ili vyombo hivyo vifanye kazi ya kutengeneza madawati yanayotarajiwa kuwa zaidi ya 120,000 ambayo yatasambazwa katika shule ili kukabiliana na tatizo la wanafunzi wanaokaa chini kwa kukosa madawati.
Hundi Kifani ya fedha hizo imekabidhiwa kwa Mheshimiwa Rais na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Akson, ambaye amesema Ofisi ya Bunge imetekeleza wito wa serikali wa kubana matumizi ambapo kiasi hicho cha shilingi Bilioni 6 kimepatikana kwa kipindi kifupi cha takribani nusu mwaka.
Katibu wa Bunge Dkt. Thomas Kashilila ametaja maeneo ambayo Bunge limebana matumizi kuwa ni Safari za nje ya nchi, Mafunzo nje ya nchi, Machapisho na ununuzi wa majarida, Shajala, Chakula na Viburudisho, Mtandao, Malazi hotelini, Matibabu ya wabunge na familia zao nje ya nchi, Umeme, Maji, Simu na Uendeshaji wa Mitambo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli pia ametengua uteuzi wa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga  Bi. Anne Kilango Malecela na Katibu Tawala wa Mkoa huo Bw. Abdul Rashid Dachi, kufuatia mkoa huo kutoa taarifa zisizo sahihi kuwa hauna watumishi hewa.
Rais Magufuli ametangaza kutengua uteuzi wa Viongozi hao wa Mkoa wa Shinyanga leo tarehe 11 Aprili, 2016 Ikulu Jijini Dar es salaam, mara baada ya kupokea Taarifa ya Mwaka 2014/2015 ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), na kupokea hundi kifani ya shilingi Bilioni 6 kutoka Ofisi ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zilizotokana na kubana matumizi.
Dkt. Magufuli ameeleza kuwa baada ya kupata taarifa kuwa Mkoa wa Shinyanga hauna watumishi hewa, aliamua kutuma timu ya ukaguzi iliyokwenda kufanya uchunguzi ambapo hadi kufikia jana tarehe 10 Aprili, 2016 imebaini kuwepo watumishi hewa 45 huku zoezi likiwa linaendelea katika wilaya mbili za Ushetu na Shinyanga Vijijini.
“Na wale wote wa Shinyanga ambao walisemekana ni zero, hakuna mtumishi hewa, walikuwa tayari wameshalipwa shilingi milioni 339.9, nimejiuliza sana, na nikajiuliza sana na kwa kweli nimejiuliza sana na kwa masikitiko makubwa, kwa nini Mkuu wa Mkoa alisema hakuna mtumishi hewa?” Amesisitiza Rais Magufuli
Rais Magufuli amesema baada ya kutengua uteuzi wake, Anne Kilango Malecela atapangiwa kazi nyingine.
Pamoja na hatua hiyo, Dkt. Magufuli ametaka wakuu wa mikoa yote wawafichue watumishi hewa wote ili waondolewe mara moja, na ameagiza timu iliyofanya uchunguzi Mkoani Shinyanga itumike kufanya uchunguzi katika mikoa mingine kwa lengo la kukomesha upotevu mkubwa wa fedha za umma.
Katikati ya Mwezi Machi, 2016 Rais Magufuli aliwaagiza wakuu wa mikoa yote nchini kusimamia zoezi la kuwaondoa watumishi hewa wote katika orodha ya malipo ya mshahara, ambapo mpaka tarehe 31 Machi, 2016 Jumla watumishi hewa 5,507 walibanika.
Kati ya shilingi Bilioni 583 ambazo serikali imekuwa ikitumia kila mwezi kwa ajili kulipa mishahara, kati ya shilingi Bilioni 53 na 54 zimekuwa zikipotea kutokana na kulipa mishahara ya watumishi hewa.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam
11 Aprili, 2016

RAIS DKT. MAGUFULI APOKEA TAARIFA YA MWAKA YA UTENDAJI WA TAASISI YA TAKUKURU PAMOJA NA HUNDI KIFANI YA SH. BILIONI 6 KUTOKA BUNGE BAADA YA KUBANA MATUMIZI.


MLO1
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Taarifa ya Mwaka ya utendaji wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi hiyo Kamishna Valentino Mlowola Ikulu jijini Dar es Salaam.

ziara ya waziri mkuu Ruangwa kipigwa story na wakazi wa mji huo.

MER1
Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary  Majaliwa  (wapilinkulia)  akitoa msaada wa shuka na mito kwa wazazi wote waliojifungua na waliokuwa wakisubiri kujifungua kwenye wodi ya wazazi ya hospitali ya wilaya ya Ruangwa  Aprili 11, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

UKATILI WA KINSIA SOKO LA TABATA MUSLIM JIJINI DAR ES SALAAM WAPUNGUA KWA MSAADA WA SHIRIKA LA EfG.

Msaidizi wa kisheria katika soko la Tabata Muslim, Aisha Juma akizungumza wakati akifungua tamasha la kuongezea

Droo ya Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho (Azam Sports


Droo ya Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup), inatarajiwa kufanyika kesho Jumanne saa 3 usiku moja kwa moja (live) kupitia kituo cha luninga cha AzamTwo.

RAIS DK. MAGUFULI ATENGUA UTEUZI WA MKUU WA MKOA WA SHINYANGA, ANNE KILANGO MALECELA RAIS DK. MAGUFULI ATENGUA UTEUZI WA MKUU WA MKOA WA SHINYANGA, ANNE KILANGO MALECELA

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk John Pombe Magufuli ametengua uteuzi wa mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Anne Kilango Malecela kutokana na kutoa taarifa za uongo kuwa mkoa huo haukuwa na watumishi hewa.

Manny Pacquiao amchapa Tim Bradley.





Image copyright

Bondia Mfilipi.no Manny Pacquiao amemchapa bondia kutoka Marekani Tim Bradley katika pigano lake la mwisho.

Leicester City yaendeleza ubabe wao kwenye ligi ya EPL.



Image copyrightGetty
Image caption

Ligi kuu ya soka ya England imeendelea tena jumapili kwa michezo mitatu ,Sunderland wakicheza nyumbani dhidi ya vinara wa ligi Leicester city, waliambulia kipigo cha mabao 2-0, na kuwafanya leicester city kufikisha alama 72 katika Msimamo.

Ulikosa kuziona picha za mechi ya jana kati ya azamu fc na Esperance.

Image caption
Michuano ya kombe la shirikisho Afrika imeendelea tena Jumapili kwa michezo kadhaa ,Azam fc wakicheza nyumbani Azam complex jijini Dar es salaam walifanikiwa kuwachapa Esperance ya Tunisia mabao 2-1.

Bondia Anthony atamba kupigana na Fury.



Image copyrightGetty
Image caption

Bondia Anthony Joshua amesema sasa macho na akili zake anazielekeza kwa bondia Tyson Fury hii ni baada ya kushinda mkanda wa IBF wa dunia uzani wa Heavyweight siku ya Jumamosi na katika raundi ya pili ya mtoano ya dhidi ya mpinzani Charles Martin.

Je? wajua Mourinho akataa kazi syria story ipo hapa.

Mourinho


Image copyrighteutersImage captio

Aliyekuwa meneja wa klabu ya Chelsea Jose Mourinho amekataa ombi la kumtaka awe meneja wa timu ya taifa ya Syria, wakala wake amesema.

Je? wajua msimamo wa ligi ya EPL ratiba nzima ipo hapa.

Jedwali la msimamo wa ligi ya EPL kufikia 11 Aprili, 2016.

Darfur kupiga kura ya maoni leo


Image capti
Kura ya maoni itaamua kama Darfur itakuwa na majimbo matano au jimbo moja, ambapo raia watakuwa na siku mpaka ya jumatano kuamua.

Je unapenda kula samaki Plastiki yakumbwa na Samaki


Image caption
Je unapenda kula samaki ?
Ikiwa unapenda Dagaa Pweza,Pelege,Mwatiko, Papa, Kiduwa, Kambale,Tilapia ama samaki wa aiana yeyote yule basi unapaswa kusoma taarifa hii ya utafiti.

Mwanahabari wa al-Shabab auawa Somalia



ShababImage copyrightReuters
Image captionHanafi alikuwa afisa wa habari wa kundi la al-Shabab

Mwanahabari aliyesaidia kundi la al-Shabaab kuua wanahabari wenzake nchini Somalia ameuawa.
Hassan Hanafi ameuawa kwa kupigwa risasi mapema asubuhi baada ya kuhukumiwa kifo na mahakama ya kijeshi nchini humo.

KAJUNASON ASHEREKEA SIKU YAKE ZA KUZALIWA NA WATOTO YATIMA WA KITUO CHA SOS CHILDREN’S VILLAGE TANZANIA


 Mmiliki wa Kajunason Blog, Cathbert Angelo Kajuna (mwenye shati nyeupe) akimkabidhi mwakilishi wa kituo cha SOS Children’s Village Tanzania Bi. Sherry Mavura (wa kwanza kulia) msaada wa vitu mbali mbali ikiwemo Sabuni, Unga, Mchele, Mafuta, miswaki, dawa za meno kwa ajili ya kuwasaidia kuendesha kituo hicho.

Aunt Ezekiel afunguka makubwa juu ya Serikali ya JPM

 Staa wa sinema za Kibongo, Aunt Ezekiel Grayson.

Dar es Salaam: Mnyoosho! Kaulimbiu ya Rais Dkt John Pombe Magufuli ‘JPM’ ya kutumbua majipu na watu wasiolipa kodi imemdondokea staa wa sinema za Kibongo, Aunt Ezekiel Grayson baada ya gari lake aina ya Audi kukamatwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa tuhuma za kuingizwa nchini kinyemela bila kulipiwa ushuru na kukwepa kodi.

Kama ulikosa na hukupata undani wa story ya kifo cha Ndanda kasovo

Ndanda Kosovo ‘Kichaa’ enzi za uhai wake.

Dar es Salaam: Msiba! Tasnia ya Muziki wa Dansi Bongo imegubikwa na simanzi nzito kufuatia kifo cha aliyewahi kutikisa vilivyo kwa rap na vibao vikali, mwenye asili ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Ndanda Kosovo ‘Kichaa’ aliyefikwa na umauti wikiendi iliyopita, Wikienda limechimba undani wa habari hiyo.

Azam fc yawatembezea kichapo cha mbwa mwizi waarabu wa jangwani.


AZAM FC imejiweka kwenye nafasi ya kwenda hatua ya mchujo wa kuwania kupangwa kwenye makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Niyonzima afanya makubwa yanga unajua yapi yapo hapa.

Kiungo wao mchezeshaji Mnyarwanda, Haruna Niyonzima amepona malaria na tayari ameanza mazoezi.

Watuhumiwa wa Dawa za kulevya wazidi kubanwa.

maj2
WAZIRI Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa, Kassim Majaliwa amemtaka Mkuu wa Magereza mkoa wa Lindi, kuhakikisha hakuna mtuhumiwa wa dawa za kulevya atakayetoweka katika gereza la 
mkoa huo.
Amesema kuna watuhumiwa wa dawa za kulevya ambao wanahifadhiwa katika gereza la mkoa wa Lindi hivyo ni vema akajiridhisha kama ulinzi na usalama wa watuhumiwa hao umeimarishwa.
Hata hivyo, Waziri Mkuu, Majaliwa amemtaka mkuu wa gereza hilo kuwa makini na baadhi ya zabuni wanazozitoa kutoka nje na kuhakikisha ulinzi unaimarisha wakati wote gerezani hapo.