Tuesday, 3 May 2016

Stori,Prince alitaka kuwa mwalimu wa Chris Brown Kabla ya kifo chake.

Kwa mujibu wa mahojiano na jarida la Rolling Stone ambayo yalichapishwa hivi karibuni, marehemu Prince alitaka sana kuwa mwalimu wa kipaji cha Chris Brown.

WAKO TAYARI KWA AJILI YA STAND UNITED LEO, PLUIJM AKUBALI KILA KITU.


Kikosi cha Yanga kipo tayari kwa ajili ya mechi dhidi ya Stand United ya mjini Shinyanga.

RASHFORD ABEBA TUZO YA VIJANA CHINI YA MIAKA 18 NDANI YA MANCHESTER UNITED


Kinda Marcus Rashford ndiye mwanasoka bora kijana kwa wale walio chini ya umri wa miaka 18 katika klabu ya Manchester United kwa msimu wa 2015-16.

DE GEA, SMALLING WAIBUKA WACHEZAJI BORA WA MANCHESTER UNITED.


David de Gea ameteuliwa kuwa mwanasoka bora wa mwaka wa Manchester United aliyeteuliwa na mashabiki wakati beki Chris Smalling ameteuliwa kuwa mwanasoka bora kutoka ndani ya klabu.

Jaji afuta rekodi ya Kesi ya Kanye West ya kumdunda Paparazzi.

Jaji amekubali rekodi ya kitendo na hukumu ya kitendo cha Kanye West kumpiga Paparazzi kifutwe kwenye rekodi ya maisha ya rapa Kanye West.

Picha,Jumba alilonunua French Montana kutoka kwa Ex wa Justin Bieber,Selena Gomez.


Rapa French Montana amenunua jumba la Selena Gomez huko Calabasas, California kwa kiasi cha pesa Dola milioni $3.3 za Kimarekani.

Makonda Awasainisha Mikataba ya Kutafuta Watumishi HEWA Wakuu wote wa Idara Jiji la Dar es Salaam.

MKUU wa Mkoa wa Dares Salaam, Paul Makonda amewasainisha mkataba wakuu wote wa idara kusimamia na kuhakikisha hakuna mtumishi hewa atakayebainika kwenye idara zao.

Jaji afuta rekodi ya Kesi ya Kanye West ya kumdunda Paparazzi.

Jaji amekubali rekodi ya kitendo na hukumu ya kitendo cha Kanye West kumpiga Paparazzi kifutwe kwenye rekodi ya maisha ya rapa Kanye West.

KATIBU MKUU WIZARA YA MALIASILI NA UTALII,MEJA JENERALI GAUDANCE MILANZI AWASILI MKOANI KATAVI KWA AJILI YA KUFUNGA MAFUNZO YA MFUMO WA JESHI USU KWA WAHIFADHI WA SHIRIKA LA HIFADHI ZA TAIFA (TANAPA)

Ndege ndogo ya Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) iliyombeba Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Meja Jenerali Gaudance Milanzi ikiwasili katika uwanja wa ndege wa Mpanda ,Meja Jenerali Milanzi anatarajia kufunga rasmi Mafunzo ya Mfumo wa Jeshi Usu kwa Wahifadhi na Askari waajiriwa wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) yaliyofanyika katika Kambi ya Mlele iliyopo Hifadhi ya Taifa ya Katavi.

Aliyejifungua Watoto 3 Anaomba Asaidiwe kwani naye ni Mgonjwa wa Pumu.

MKAZI wa Kijiji cha Mapinduzi Kata ya Kigwe Wilaya ya Bahi mkoani Dodoma Julietha Sokoine (24) amejifungua watoto wa watatu na ameiomba serikali, taasisi,mashirika na watu binafsi kumpatia msaada wa kifedha utakaomsaidia kuwatunza watoto hao.

EDEN HAZARD AWAPATIA UBINGWA WA UINGEREZA TIMU YA LEICESTER CITY.


Timu ya Leicester City imeshinda ubingwa wa Ligi Kuu ya Uingereza kwa mara ya kwanza na kuweka historia kubwa ya mchezo wa soka nchini humo.

Wasafi Wadaiwa Kumpora Producer Frag Ngoma ya 'Bado' iliyoibwa na Harmonize Feat. Diamond.

Producer Frag kutoka Uptown Music ametumbua jipu baada ya kuibuka na kusema kuwa yeye ndiye aliyetengeneza wimbo wa Bado wa Harmonize na Diamond.

MPIGA NGOMA WA MAGIC SYSTEM AFA MAJI NCHINI IVORY COAST.

Mpiga ngoma wa bendi maarufu ya muziki ya Magic System nchini Ivory Coast amekufa maji akiwa na umri wa miaka 46, taarifa ya kwenye Facebook ya kundi hilo imesema.

Rais wa Zanzibar Dr. Ali Mohamed Shein Aapishwa Rasmi Kuwa Mjumbe wa Baraza la Mawaziri.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein leo asubuhi tarehe 02 Mei, 2016

Siri Kuu Kuhusu Escrow zafichukastory nzima ipo hapa.

SIRI kuu ya James Rugemalira, kumwaga mabilioni ya shilingi kwa baadhi ya majaji wa mahakama kuu, viongozi waandamizi serikalini na madhehebu ya kidini, wabunge na viogogo wa Ikulu, zimeanza kufumuka.

MAPOROMOKO YA ARDHI WILAYA YA MOSHI YAMSHTUA MBUNGE WA JIMBO LA VUNJO ,JAMES MBATIA.

Mbunge wa Jimbo la Vunjo akisalimiana na mmoja wa waathirika wa mvua kubwa iliyonyesha hivi karibuni na kusababisha kufusi kilichokuwa kando ya nyumba yake kuporomoka na kuhatarisha maisha yake katika kijiji cha Iwa ,Kirua Vunjo katika wilaya ya Moshi.

Mwanamuziki Asifiwa na Wengi Kwa Kufanya Hili Jambo...

Wanasema ukipenda boga, penda na maua yake.
Kwa Diamond kumpenda Zari the Bosslady kunaamanisha kuyapenda pia maua yake matatu ya mwanzo. Unapompenda mwanamke ambaye tayari ana watoto watatu kabla yako, ni lazima ukutane na changamoto nyingi hasa za kutengeneza ukaribu na

WAKAZI WA NEWCASTLE UNITED WAPIGA POMBE KUPINDUKIA MEI MOSI KIASI.

Mitaa ya mji wa Newcastle nchini Uingereza ilijaa vioja vilivyotokana na wakazi wake kunywa pombe kupita kiasi na kushindwa kujimudu katika mapumziko ya mwishoni mwa wiki ya Mei Mosi.

WADAU WA HABARI NCHINI WAJADILI CHANGAMOTO ZINAZOWAKABILI.

Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA) tawi la Tanzania, Simon Berege, akitoa salamu za ufunguzi katika Maadhimisho ya Siku ya  Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani 2016 yanayofanyika Kitaifa katika Hotel ya Malaika Beach Resort Jijini Mwanza.

NEC YAKAMILISHA RASIMU YA KWANZA YA TAARIFA YA UCHAGUZI MKUU WA OKTOBA 2015

lubuva

Kamati Maalum iliyoundwa kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa ajili ya kuandaa Taarifa ya Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani uliofanyika nchini Oktoba 25, 2015 imekamilisha Rasimu ya kwanza ya Taarifa hiyo na kuiwasilisha kwa Tume.
 
Akizungumza Katika kikao cha Tume mara baada ya kupokea Rasimu hiyo ya kwanza,

Beyonce na Jay Z Wafanya yao makubwa huko new york.

Beyonce na Jay Z waliamua kufanya uamuzi wa pamoja wa kuzusha tetesi za kuachana kwa lengo la kutengeneza pesa.

MBUNGE ABDALLAH ULEGA ADHAMIRIA KULIKOMBOA JIMBO LA MKURANGA KIMAENDELEO.

ul001
Mbunge wa jimbo la Mkuranga Mh. Abdallah Ulega akichangia Bajeti ya Serikai katika Mpango pili  wa wa miaka mitano ijayo wakati wa vikao vya bunge la bajeti linaloendelea mjini Dodoma hivi karibuni.

Gigy money afanya mambo hadharani apiga mtu mabusu ya kutosha wema hoi.

Picha zinazomuonesha Gigy Money wakati akimpiga mabusu Idris Sultan wakiwa katika show ya Pool Party iliyofanyika Ijumaa iliyopita katika hotel ya Regency Park jijini Dar es salaam, zinawatoa povu mashabiki wa Wema Sepetu.

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumanne ya May 3.

Kichwa Cha Binadamu Kuanza Kupandikizwa kwa Operation Kwenye Mwili wa Mtu Mwingine.

Mtaalam wa upasuaji wa mfumo wa neva (neurosurgeon) Sergio Canavero kutoka nchini Italia, anakusudia kufanya jaribio la kwanza la kupandikiza kichwa cha binadamu kwenye mwili wa binadamu mwingine, ifikapo mwakani.

Wataalam wengi wa upasuaji wanafikiria wazo hilo ni la kiuwendawazimu, lakini sio kwa mtaalamu huyo, kwani anasema bado anapanga kujaribu pandikizo la kwanza la kichwa kwa binaadamu. (Head Transplant)

Dk. Canavero ambaye mpaka sasa ameshapata mtu wa kujitolea kufanya zoezi hilo, kijana mwenye asili ya Urusi ambaye ni mtaalam wa software Valery Spiridonov, ambaye ana tatizo la kupoteza nguvu kwa misuli yake ya mwili.

Dk. Canavero amesema mafanikio yake yameonesha kuwa mpango wake wa kupandikiza kichwa cha binadamu kwa mwili wa mtoaji (donor) bado upo, na ataanza mpango huo mwishoni mwa mwaka 2017 na unaweza kuwa njia ya kutibu waliopooza mwili.

“Ningesema tuna takwimu nyingi zinaendelea, ni muhimu kwa watu kuacha kufikiria jambo hili sio rahisi, hii inawezekana kabisa na tunaendelea kulifanyia kazi”, alisikika Dk, Canavero akimwambia mwanasayansi mchanga.

Timu iliyo nyuma ya kazi hiyo ilipost video ikimuonesha nyani ambaye alifanyiwa upandikizwaji huo, na kufanikiwa kutembea baada ya uti wa mgongo kutenganishwa na kuunganishwa tena'
Upandikizwaji wa kichwa kwa nyani ulifanywa katika chuo cha Harbin nchini China ( Harbin Medical University) na kufanikiwa kwa kiasi kikubwa, bila kuwa na muathiriko wowote katika uti wa mgongo, lakini aliuawa baada ya masaa 20 baadaye, kutokana na sheria za kazi.

Dk. Canavero amesema atahitaji pesa nyingi ili kuwalipa timu ya upasuaji, kwa mtu wa kwanza ambaye ni raia wa Urusi, hivyo amemuomba mwanasayansi tajiri zaidi Mark Zuckerberg, kufadhili upasuaji huo.

Picha ya Nyani aliyepandikizwa kichwa.
Kijana Valery Spiridonov aliyejitolea kufanyiwa upandikizwaji huo wa kwanza, ambaye mwili wake una tatizo la misuli.