Tuesday, 3 May 2016

KATIBU MKUU WIZARA YA MALIASILI NA UTALII,MEJA JENERALI GAUDANCE MILANZI AWASILI MKOANI KATAVI KWA AJILI YA KUFUNGA MAFUNZO YA MFUMO WA JESHI USU KWA WAHIFADHI WA SHIRIKA LA HIFADHI ZA TAIFA (TANAPA)

Ndege ndogo ya Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) iliyombeba Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Meja Jenerali Gaudance Milanzi ikiwasili katika uwanja wa ndege wa Mpanda ,Meja Jenerali Milanzi anatarajia kufunga rasmi Mafunzo ya Mfumo wa Jeshi Usu kwa Wahifadhi na Askari waajiriwa wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) yaliyofanyika katika Kambi ya Mlele iliyopo Hifadhi ya Taifa ya Katavi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Meja Jenrali Gaudance Milanzi akipokelewa na mwenyeji wake Mkurugenzi wa Shirika la Hifadhi za Taifa nchini (TANAPA) Allan Kijazi alipowasili katika uwanja wa ndege wa Mpanda mkoani mkoani Katavi kwa ajili ya shughuli ya kufunga Mafunzo hayo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Meja Jenerali Gaudance Milanzi akizungumza jambo na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Allan Kijazi mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Mpanda
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Meja Jenerali Gaudance Milanzi akisalimiana na Kaimu Mkurugenzi wa Uhifadhi wa Shirika la Hifadhi za Taifa nchini (TANAPA) Mtango Mtahiko

No comments: