Saturday, 16 April 2016

Tazama Show Nzima ya Navy Kenzo Walivyoipeleka Kamatia Chini Mjini Dodoma..Mtwara Week End Hii Kaeni Tayari


Kamatia Chini Lights Up Tour ya kundi la muziki wa bongofleva

RAIS DK. JOHN POMBE MAGUFULI KATIKA MATUKIO ZAIDI UZINDUZI WA (FLYOVER) MAKUTANO YA BARABARA YA MADELA NA NYERERE

 Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akilakiwa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano  Profesa Makame Mbarawa  alipowasili kuweka jiwe la msingi la mradi wa ujenzi wa barabara ya juu kwenye makutano ya barabara za Mandela na Nyerere maeneo ya Tazara Jijini Dar es Salaam leo Jumamosi Aprili 16, 2016.

Vitu vimewahi kumtokea Nisha nchini China na hawezi kuvisahau. Vitu vimewahi kumtokea Nisha nchini China na hawezi kuvisahau.

Mwigizaji wa bongo movie Salma Jabu a.k.a Nisha kwa sasa atakua anaonekana sana China na nyumbani Tanzania na hii ni baada ya kuamua kwenda kusomea masomo ya Ujasiriamali China masomo ambayo yatachukua miezi mitatu kuhitimu.

Godzilla na Mwasiti wanayo furaha kukualika kuisikiliza hii single mpya…

Ni siku kadhaa tangu rapper Godzilla aichie single yake iitwayo ‘I Get High’, sasa time hii anakualika kuisikiliza hii single mpya inayoitwa First Class aliyomshirikisha Mwasiti.

DART YAHIMIZWA KUELIMISHA WAKAZI WA DAR.


Dart4_zps86ebdba6
ZIKIWA zimebaki siku chache kabla ya mradi wa mabasi yaendayo kasi kuanza, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewaagiza wakuu wa taasisi zinazohusika na utekelezaji wa mradi huo kuhakikisha wanatoa elimu kwa umma ili kupunguza madhara yanayoweza kujitokeza.

TFF YATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI MZFA .


Shirkisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limetuma salamu za rambirambi kwa Chama cha Mpira wa Miguu mkoa wa Mwanza (MZFA), kufuatia kifo cha aliyekuwa Mwenyekiti mstaafu wa MZFA na makamu mwenyekiti wa FAT Silvanus Makalu Ngofilo aliyefariki dunia juzi jijini Mwanza.

Bunge kuanza kutumia mfumo mpya wa kurusha matangazo kwa njia ya Satellite.


Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limefanya mabadiliko ya kurusha matangazo yake ambayo yanaviwezesha vyombo vya habari (redio na tv) kupata matangazo hayo moja kwa moja bila kufunga mitambo yao katika eneo la bunge.

Bibi Kizee Abakwa Mkoani Singida


Pichani ni Bibi kizee mwenye umri wa miaka 84 na mkazi wa Kijiji cha Chungu, tarafa ya Ihanja, wilaya ya Ikungi, Mkoani Singida

Mabasi Yaendayo kasi Kuanza Mei 10.



Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais anayeshughulikia Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, George Simbachawene amesema mradi wa Mabasi Yaendayo Kasi (Dart), unatarajia kuanza rasmi Mei 10, mwaka huu. 

Kama ulikuwa hujui kuwa Kunywa Maji ya Moto ni Tiba ya Magonjwa Mengi....

Kuna tiba nyingi za kitabibu, zilizogawanyikaa katika makundi mbalimbali. Kuna zile za hospitali ambazo ni lazima zinunuliwe, lakini kuna tiba ambazo kwa ushauri wa daktari hata wewe unaweza kuziandaa bila kutumia gharama kubwa.

Waziri wa Ardhi,Nyumba na Makazi William Lukuvi Aziponda Nyumba Zinazojengwa na NHC,PPF.

WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi, amesema hakuna taasisi ya Serikali wala binafsi nchini iliyojenga nyumba za bei nafuu.

BUNGE Latoa Tamko Kuhusu Taarifa za Uzushi Zinazosambaa Kuhusu Mkataba wa Lugumi.


Kumekuwa na taarifa zinazoendelea kupotosha umma na baadhi ya vyombo vya Habari kuwa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) ilipokuwa ikitekeleza majukumu yake tarehe 5 Aprili, 2016 ililitaka Jeshi la Polisi kuwasilisha Mkataba ulioingiwa Kati ya Jeshi hilo na Kampuni ya Lugumi Enterprises Ltd kuhusu mradi wa Utambuzi wa Alama za Vidole AFIS (Automated Fingerprint Identification System).

SOMA Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumamosi Ya April 16, Ikiwemo ya Bunge Kuufyata Mkataba wa Lugumi.


SOMA Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumamosi Ya April 16.

Meneja wa Q Chief na MB Dog Afunguka...Nimeshatumia zaidi ya Bilioni Moja Kuwasaidia Wasanii.

Mkurugenzi wa label ya ‘QS Mhonda Entertainment’ QS Mhonda amesema toka aanze harakati za kusimamia muziki tayari ameshatumia zaidi ya bilioni 1.
234

Jack Wolper Adaiwa Kutolewa vyombo nje na Mwenye Nyumba......

STAA wa filamu Bongo, Jacqueline Wolper ambaye hivi karibuni ameonekana kulegalega amedaiwa kutolewa vyombo vyake nje kwenye nyumba aliyokuwa amepanga maeneo ya Mikocheni jiji Dar.

Utafiti: 71% ya Watanzania Hutumia Muda wao Katika Mambo yasiyo na Maana...

Utafiti uliofanyika hivi karibuni na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) umebaini kwamba asilimia 71 ya watanzania wanatumia muda mwingi kufanya shughuli zisizokuwa za uzalishaji mali wala tija binafsi kwao na kwa Taifa kwa ujumla.

J wajua kilicho mkuta Aunt Ezekiel Afungukia Kuachana na Moses Iyobo.


KUFUTAIA kuwepo kwa taarifa kuwa Mwigizaji Aunt Ezekiel amempiga chini mpenzi wake Moses Iyobo, mrembo huyo ameibuka na kusema taarifa hizo hazina ukweli.

MPYA Kuhusu Mradi wa Mabasi Yaendayo Kasi (Dart)...Tarehe ya Kuanza Kazi Yatajwa Rasmi...

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais anayeshughulikia Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, George Simbachawene amesema mradi wa Mabasi Yaendayo Kasi (Dart), unatarajia kuanza rasmi Mei 10, mwaka huu.

Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) yakana Ulinzi wa Makapuni Binafsi Kwenye Sehemu Nyeti.


Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) imesema kuwa makampuni binafsi ya ulinzi yanayofanya kazi bandarini hayahusiki na ulinzi wa sehemu nyeti za za Mamlaka hiyo.

Mange Kimambi Afunguka Makubwa Kuhusu Taarifa za Kijana Kukamatwa na Polisi Baada ya Kumuita Rais 'Bwege'

Blogger Maarufu kwa kuikosoa serikali na mambo mengine ya kijamii amefunguka maoni yake baada ya taarifa kusambaa mitandaoni kuwa kuna kijana amekamatwa na polisi mkoania Arusha kwa kosa la kumwita Rais Bwege kupitia mtandao wa Facebook....

TETEMEKO LENYE NGUVU LAIKUMBA TENA JAPAN.

Tetemeko lenye nguvu limelikumba eneo la karibu na mji wa kusini mwa Japan wa Kumamoto, ikiwa ni siku moja tu baada ya tetemeko kubwa kuuwa watu wapatao tisa.

Manispaa ya Kinondoni Chini ya CHADEMA Yatangaza Neema Kwa Wakazi Wake..Sasa Kila Mkazi Kupata Bima ya Afya.

Manispaa  ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, inayoongozwa na Chama cha Demkrasia na Maendeleo (Chadema), chini ya Ukawa imeanza kazi kwa staili ya aina yake baada ya kutangaza neema ya bima ya afya kwa wananchi wa Manispaa hiyo.

PAPA FRANCIS KWENDA KUWAUNGA MKONO WAHAMIAJI.

Papa Francis anatarajiwa kutembelea kisiwa cha Ugiriki cha Lesbos kuuwaunga mkono wakimbizi wanaojaribu kufika nchi za Ulaya.

PAPA FRANCIS KULA MLO WA MCHANA NA WAKIMBIZI 250 NCHINI UGIRIKI.

Papa Francis amewasili katika kambi iliyopo kwenye kisiwa cha Ugiriki cha Lesbos kuwaunga mkono wakimbizi wanaojaribu kuingia mataifa ya Ulaya.

Tuhuma za Mwanamuziki TID Kutumia Madawa ya Kulevya...Mwenyewe Afunguka.

Baada ya KR kujitambulisha kuwa yeye ndiye Rais wa RADA Entertainment na Juma Nature kumpinga kwa kejeli akisema hamtambui Rais yoyote zaidi ya Rais Magufuli hatimaye TID anyoosha maelezo.

LEMUTUZ Afunguka Kuhusu Kijana Aliyekamatwa Arusha Kwa Kumwita Rais Bwege..Ailaumu Serikali na Polisi.

 Blogger Lemutuz naye amefunguka kuhusu kijana aliyekamatwa na Polisi kwa tuhuma za kutumia Mtandao wa Facebook kumwita Rais Magufuli Bwege  na kwamba hawezi kufananishwa na Nyerere..

Wafanyakazi ‘waufagilia’ ujenzi Daraja la Kigamboni.

da
Mmoja wa wataalamu wa kizalendo walioshiriki kwenye ujenzi wa Daraja la Kigamboni Muhandisi Jamal Mruma (kushoto) akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) namna mradi huo ulivyowajengea uwezo kiutendaji wafanyakazi wazalendo. Kulia ni Meneja wa Mradi huo huo Bw. Zhang Bang Xu.

WAZIRI WA UJENZI ATEMBELEA OFISI YA MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA (TCRA) NA KUTOA MWONGOZO WA UTENDAJI KAZI.

3 
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa, akifafanua jambo wakati akizungumza na Wafanyakazi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) (hawapo pichani), kuhusu mkakati mpya wa Mamlaka hiyo wa kufanya kazi kwa ubunifu na uadilifu ili kuongeza mapato.

NAPE AFANYA ZIARA MKOANI MARA NA SHINYANGA.

 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akizungumza na washika dau wa Habari, Utamaduni Sanaa na michezo wa mkoa wa Mara ikiwa sehemu ya ziara yake ya kukutana na wadau hao wakiwemo watumishi wa serikali .
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye leo ameendelea na ziara yake katika mkoa wa Mara na Shinyanga ambapo alikutana na Watumishi na wadau walio chini ya Wizara yake.

WAZIRI WA AFYA,MAENDELEO YA JAMII,MH.UMMY MWALIMU AMEANZA ZIARA YA KIKAZI YA SIKU MBILI MKOANI SHINYANGA.

6 
Waziri wa afya akisalimiana na watumishi wa ofisi ya mkuu wa shinyanga.

MKURUGENZI WA HALMASHAURI WA MJI KAHAMA APEWA SIKU TISINI NA WAZIRI WA AFYA UMMY MWALIMU AWE AMENUNUA MASHINE YA MIONZI X RAY.

1 
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto akiongea na baadhi ya wakazi wa kahama waliofika hospitalini hapo kuangalia wagonjwa wao.

Nape:Nitarudisha heshima ya Tasnia ya Habari nchini.


P3 
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye akizungumza na wadau waliopo chiniya wizara yake pamoja na watumishi wa sekretarieti ya mkoa wa Mara wakati wa ziara ya kutembelea maeneo yanayohusu sekta za wizara, kupokea taarifa ya mkoa na kuwapatia  vitendea kazi  maafisa mawasiliano wa mkoa huo. Wengine pichani ni Katibu Tawala mkoa wa Mara Bw.Benedict Ole Kuyan(wa kwanza kulia),Mkuu wa wilaya ya Butiama Bi.Anarose Nyamubi(wa tatu kulia) na Kaimu meya wa manispaa Bw.Wambura Kajala.

EALA TANZANIA WAKUTANA NA KAMATI ZA BUNGE LA TANZANIA.

1Mwenyekiti wa Wabunge wa Afrika Mashariki kutoka Tanzania, (EALA), Makongoro Nyerere akifafanua jambo wakati wabunge kutoka EALA walipokutana na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje na Ulinzi na Usalama pamoja na Kamati ya Viwanda Biashara  na Mazingira jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kadumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Adadi Rajabu na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira, Dk. Dalali Kafumu.

MKURUGENZI WA HALMASHAURI WA MJI KAHAMA APEWA SIKU TISINI NA WAZIRI WA AFYA UMMY MWALIMU AWE AMENUNUA MASHINE YA MIONZI X RAY.


Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto akiongea na baadhi ya wakazi wa kahama waliofika hospitalini hapo kuangalia wagonjwa wao.

INAFRIKA BAND YAFANYA KWELI NASHVILLE, TENNESSEE.

Wanamuziki wa bendi ya Inafrika toka Tanzania wakipata picha ya kumbukumbu Nashville jimbo la Tennessee ambapo wapo tangia March 18, 2016mpaka April 18, 2016 kwenye tamasha linaloandaliwa kila mwaka na Dolly Parton linalofanyika kwenye park iitwyo Dollywood iliyopo mjini humo. Tamasha hilo hushirikisha bendi mbalimbali kutoka mabara yote, Bara la Afrika liliwakilishwa na Inafrika Bendi kutoka Tanzania.