Papa Francis anatarajiwa kutembelea kisiwa cha
Ugiriki cha Lesbos kuuwaunga mkono wakimbizi wanaojaribu kufika nchi
za Ulaya.
Papa Francis ambaye atakutana na kiongozi wa Orthodox, Patriarch Bartholomew, atatembelea kambi ya watu zaidi ya 3,000 wanaongojea ama wapatiwe hifadhi ama warejeshwe Uturuki.
Kisiwa cha Lesbos kimekuwa ni eneo muhimu la kuingilia Ulaya kwa wahamiaji katika mwaka uliopita.
Maelfu sasa wamekwama katika kisiwa hicho baada ya mwezi uliopita Umoja wa Ulaya na Uturuki kuingia makubaliano ya kupunguza tatizo la wahamiaji.
No comments:
Post a Comment