Waziri
wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto akiongea na baadhi ya
wakazi wa kahama waliofika hospitalini hapo kuangalia wagonjwa wao.
Waziri.Ummy Mwalimu akitoa angalizo kwa wagonjwa waliofika kupata matibabu kwenye hospitali ya rufaa ya mkoa wa.shinyanga
Mh.Ummy
Mwalimu akiwaelekeza kamati ya afya ya wilaya ya kahama mahali
linapotakiwa kuwekwa bango linaonesha huduma za wazee inapopatikana.
Mkuu
wa wilaya ya Kahama Mh.Vita Kawawa(Katikati) akionesha kwa vitendo
bango hilo linapotakiwa kuwekwa,kushoto ni Mh.Ummy Mwalimu na kulia ni
mkurugenzi wa halmashauri ya mji kahama Anderson Msumba.
Mfamasia
Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga, Luciano Lodrick
akimpatia maelezo waziri ,maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na watoto
jinsi ya utengenezaji wa maji tiba.
Waziri Ummy Mwalimu akiangalia kifaa cha kutengenezea maji tiba kwenye.hospitali ya.rufaa ya mkoa wa shinyanga.
Mh.Ummy
Mwalimu akiangalia matangazo yaliyobandikwa kwenye ubao hospitanini
hapo.Waziri Ummy ameuagiza uongozi wa hospitali hiyo kubandika gharama
za matibabu pamoja na namba za simu kwa ajili ya kupokelea maoni na
malalamiko toka kwa wananchi.
Mkurugenzi wa halmashauri wa mji
kahama amepewa siku tisini awe amenunua mashine ya mionzi (x ray)kwa
ajili ya hospitali ya mji kahama
Agizo hilo amepewa jana na Waziri
wa afya,maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na watoto Ummy mwalimu wakati
alipotembelea hospitali hiyo pamoja na kuongea na watumishi wa kada ya
afya wa wmji huo.
Waziri Ummy alisema ametoa agizo
hili ili kuweza kurahisisha usumbufu wanaupata wananchi wa wilaya hiyo
kwa kwenda kupata huduma nje ya hospitali ambapo wakati mwingine vipimo
hivyo vinakuwa havisomeki vizuri kwa kukosa viwango vinavyostahili za
mashine hizo.
Hata hivyo waziri ummy alisema
upatikanaji wa mashine hizo itapunguza malalamiko mengi toka kwa
wananchi kwa ukosefu wa kifaa tiba hicho ili kwani hospitali hiyo hivi
sasa inahudumia wananchi zaidi ya milioni moja hususan toka wilaya zote
za wilaya hii
Aidha, alizitaka halmashauri zote
mjini kuweza kuwekeza kwenye huduma za vifaa tiba ambavyo inarahisisha
kugundua matatizo yanayowakabili wananchi wanaofika kwenye kupata huduma
na hivyo kuwapatia matibabu stahili wagonjwa wanaofika kupata matibabu
kwenye vituo vya kutolea huduma nchini.
?siku hizi lazima muwekeze kwenye
kununua vifaa tiba ili kuweza kupata kutoa huduma nzuri ,pesa mnakusanya
na kahama ni halmashauri tajiri,mkurugenzi nakupa siku tisini uwe
umenunua mashine hiyo
Naye mkuu wa Wilaya hiyo Mh. Vita
kawawa amemuahidi waziri huyo kwamba amepokea maagizo yote aliyoyatoa na
atayafuatilia ili kuweza kutatua malalamiko ya wananchi na yale ya
watumishi wa kada ya afya.
No comments:
Post a Comment