Saturday, 16 April 2016

PAPA FRANCIS KULA MLO WA MCHANA NA WAKIMBIZI 250 NCHINI UGIRIKI.

Papa Francis amewasili katika kambi iliyopo kwenye kisiwa cha Ugiriki cha Lesbos kuwaunga mkono wakimbizi wanaojaribu kuingia mataifa ya Ulaya.

Kambi hiyo ya Moria inawakimbizi 3,000, ambao baadhi yao wanakabiliwa na hatua za kurudishwa nchini Uturuki. Papa Francis anatarajiwa kula mlo wa mchana na wakimbizi 250.

Papa Francis amesema safari yake ya Ugiriki ni ya kushuhudia janga kubwa la wahamiaji duniani kutokea tangu vita ya pili ya dunia. Papa Francis ameahidi kuwachukua wakimbizi 10.
Papa Francis akiongea na Waziri Mkuu wa Ugiriki Alexis Tsipras baada ya kuwasili kisiwa cha Lesbos
Mkimbizi akiwa na bango la kumkaribisha Papa Franis katika kisiwa cha Lesbos

No comments: