Mwigizaji wa bongo movie Salma Jabu a.k.a Nisha kwa sasa atakua anaonekana sana China na nyumbani Tanzania na hii ni baada ya kuamua kwenda kusomea masomo ya Ujasiriamali China masomo ambayo yatachukua miezi mitatu kuhitimu.
Kwenye Exclusive Interview na OnAIRwithMillardAyo Nisha amesema katika vitu hawezi kusahau ni moja ya safari zake kwenda China ambapo alisachiwa kwa zaidi ya dakika 180 kwenye uwanja wa ndege baada tu ya kutua na hiyo ni baada ya kuonekana kama anatokea Tanzania nchi ambayo baadhi ya raia wake wamekamatwa sana wakiingiza dawa za kulevya China.
Nisha amesema ‘ Iliniathiri sana kisaikolojia, siku hiyo tunasachiwa kwa Tanzania nilikua peke yangu, kulikua na wengine kutoka Brazil na Wanigeria ambao wote tulisachiwa kwa muda mrefu, walionusurika tulipita na waliobaki wakabaki…… kwa upande mwingine ishu ya mimi kuandikwa kwamba huwa nabeba dawa za kulevya wala hainisumbui sababu sio kweli kabisa‘
No comments:
Post a Comment