Waziri
wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye akizungumza na
wadau waliopo chiniya wizara yake pamoja na watumishi wa sekretarieti ya
mkoa wa Mara wakati wa ziara ya kutembelea maeneo yanayohusu sekta za
wizara, kupokea taarifa ya mkoa na kuwapatia vitendea kazi maafisa
mawasiliano wa mkoa huo. Wengine pichani ni Katibu Tawala mkoa wa Mara
Bw.Benedict Ole Kuyan(wa kwanza kulia),Mkuu wa wilaya ya Butiama
Bi.Anarose Nyamubi(wa tatu kulia) na Kaimu meya wa manispaa Bw.Wambura
Kajala.
Katibu Tawala mkoa wa Mara Bw.Benedict Ole Kuyan akizungumza na wadau
mbali mbali wa sekta za Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo pamoja na
watumishi wa serikali wa mkoa wa Mara leo hii wakati wa Ziara ya Waziri
wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye mkoani humo.Kaimu
Mkuu wa mkoa wa shinyanga Bi.Josephine Matiro akizungumza jambo wakati
wa kumkaribisha Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape
Nnauye baada ya kuwasili mkoani hapo ili kujua changamoto mbalimbali za
watumishi walio chini ya wizara yake na kuongea na wadau wa
Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo.
Waziri
wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye akipata maelezo
kutoka kwa fundi mitambo mwandamizi wa shirika la utangazaji
Tanzania(TBC) Bw.John Igomego jinsi mitambo yakurushia matangazo ya
shirika hilo inavyofanya kazi mkoa wa Mara.
Waziri
wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye akizungumza na
katibu wa chama cha mapinduzi(CCM) mkoani Shinyanga Alhaj Saad
Kusilawe(mwenye kofia ya njano) kuhusu maendelezo ya uwanja wa kambarage
ambao unamilikiwa na chama hicho mkoani hapo.Mhe.Nape amewaasa viongozi
wa mkoa huo kutafta wadhamini ili kuuboresha uwanja huo.
Waziri
wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo amesema kuwa atahakikisha heshima
ya tasnia ya habari inarudi baada ya kupitishwa kwa mswada wa sheria
ya huduma za vyombo vya Habari.
Waziri
Nape ameyasema hayo alipokuwa katika katika ziara mkoani Mara na
Shinyanga na kutembelea maeneo yanayohusu sekta za wizara hiyo na
kupokea taarifa ya mkoa na kuwapatia vitendea kazi maafisa mawasiliano
wa mikoa hiyo.
“Ule
mswada utatoa tafsiri ya mwandishi wa habari,maana mwandishi wa habari
lazma awe na sifa.Siku hizi anaweza kuwa mtu anauza ndizi alafu
akajifunza kupiga picha akajiita na yeye mwandishi wa Habari.Ukifanya
ivyo tasnia hii inakosa heshima,kwaiyo sheria ile itatafsiri nani
mwandishi wa habari”Alisema Nape.
Aidha
Waziri Nape alisema kuwa kwa kufanya hivi sheria hii itatibu tatizo la
kulipwa vibaya na wamiliki wa vyombo vya habari maana mwandishi huyu
atakuwa na elimu,maana kama hana elimu mmiliki ataajili mtu anaejua
kusema wa kijuweni alafu ndo anamuajiri anakuwa mtangazaji wa radio
yake kisa tu anajua kusema.
Pamoja
na hayo waziri uyo mwenye dhamana ya wizara nyeti ya habari alisema
kuwa sheria hiyo pia itazungumzia maslahi ya mwandishi wa
habari,itawabana wamiliki na mswada huu ukipita utarudisha heshima ya
tasnia hii ya habari katika nchi yetu.
Akizungumzia
upande wa radio kujenga nchi waziri nape amewaasa waandishi wa habari
na watangazaji wa radio kujenga amani ya nchi yetu kwa kuwaunganisha
watanzania kupitia radio zao na si kuwatenganisha akitolea mfano wa
yaliyotokea nchini Rwanda kwamba radio zilitumika kuhamasisha mauaji.
Mheshimiwa
Nape pia amehaidi kuimarisha vitengo vya mawasiliano serikalini ikiwa
ni pamoja na kuwapa maafisa hao vitendea kazi, pia ameliomba jeshi la
polisi kutoa ushirikiano katika kutoa taarifa na amehaidi kuzungumza na
jeshi hilo ili waandishi hawa waweze kupata taarifa kirahisi.
Waziri
uyo yupo katika ziara ya mikoa ya Kagera,Mara,Shinyanga,Tabora na
Singida ikiwa na lengo kuu la kuileta Wizara ya habari,utamaduni,Sanaa
na Michezo mikoani na wilayani karibu na wadau.
No comments:
Post a Comment