Monday, 2 May 2016
WAMBURA-SITAKUBALI RASILIMALI ZA TAIFA HILI ZICHEZEWE.
Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe Anastazia Wambura(wa pili kushoto) akipata msaada wakati akiteremka toka katika kiwanja cha shirika la utangazaji Tanzania(TBC) kulipojengwa nyumba za watumishi wa shirika hilo ambazo hazijaisha kwa zaidi ya miaka 20 sasa na kutoa maagizo ya kumalizia nyumba hizo au kuwapa Halmashauri ya Kisarawe ili wajenge Hostel za wanafunzi.(Picha na Daudi Manongi-WHUSM)
Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu wa shirika la utangazaji Tanzania(TBC) Bi.Joselin Lugola akitoa mrejesho kuhusu nyumba za shirika hilo zilizo kisarawe mkoani Pwani ikiwemo kukamilisha upatikanaji wa hati wa eneo hilo na kuliendeleza ili watumishi wa TBC wa kisarawe walitumie kwa makazi.
Kaimu mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Bi.Nahya Mansour(wa kwanza kushoto) akimskiliza Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe Anastazia Wambura(hayupo pichani) wakati akitoa maagizo juu ya nyumba za Shirika la Utangazaji Tanzania(TBC) zilizopo eneo la kimani Kisarawe mkoa wa Pwani.wengine pichani ni Mkurugenzi mtendaji wilaya ya Kisarawe Bi.Mwanamvua Mrindoko(wa pili kushoto).
Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe Anastazia Wambura akitoa maelekezo kwa Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu wa shirika la utangazaji Tanzania(TBC) Bi.Joselin Lugola wakati alipofanya ziara katika nyumba za shirika hilo zilizopo kisarawe mkoani Pwani.
Bora Ukimwi Kuliko Kutumia Dawa za Kulevya-Ferooz.
Subscribe to:
Posts (Atom)