Friday, 29 April 2016

HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI-MNH- YAMEKA MIKAKATI KUHAKIKISHA WATOTO WANAOZALIWA NA MATATIZO YA KUTOSIKIA WANAPATIA MATIBABU.

wa masikio Fayaz Jaffer akitoa elimu kwa wazazi / walezi , jinsi ya kutunza kifaa kinachomsaidia mtoto mwenye matatizo ya kusikia kuweza kusikia na kuwasiliana. Mtaalam huyo ametoa elimu hiyo leo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili-MNH- alipokuatana na wazazi ambao watoto wao walifanyiwa upasuaji nchini India na kuwekewa kifaa hicho.

C2 
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili –MNH- Profesa Lawrence Museru akielezea mipango ya MNH katika kuhakikisha huduma hiyo inakuja kutolewa hapa MNH kwa siku zijazo

FARID MUSSA WA AZAM FC AKIENDELEA KUPAMBANA KUPATA TIMU ULAYA, HAPA ANAFANYA MAJARIBIO

 


Cheki taswira, kinda wa Azam FC, Farid Mussa akiwa katika majaribio kuwania nafasi acheze soka la kulipwa barani Ulaya. Hapa Farid anafanya majaribio katika klabu ya Club Deportivo Tenerife Hispania. Leo ametimiza siku ya nne katika majaribio na taarifa zinasema anaendelea vizuri.

STEWART HALL, ASHANGAZWA NA YANGA, YANGA KILA KONA....


Kocha Stewart Hall wa Azam FC ‘amenunua’ ugomvi wa Yanga na Coastal Union kwa kusema kuwa kuna kila sababu ya kujifikiria mara mbili kwa nini kila siku itajwe Yanga katika matokeo tatanishi na kuongeza kuwa Yanga haikupata ushindi halali kutinga fainali ya Kombe la Shirikisho.

BARUA YA MHARIRI MKUU WA GAZETI BORA LA MICHEZO LA CHAMPIONI KWENDA KWA WASOMAJI WAKE.


JUMAMOSI iliyopita niliandika na kuelezea namna safari yangu ya kwenda Hispania ilivyokuwa na namna nilivyowaza kama ningepata nafasi ya kuhojiana na wachezaji nyota kabisa duniani kama Lionel Messi, Luis Suarez na Neymar.

SERIKALI YAZIDI KUPAMBANA NA UGONJWA WA MALARIA NCHINI.

 index
Kufanikiwa kwa juhudi za Kutokomeza ugonjwa wa Malaria kutaufanya ulimwengu kuwa mahali pazuri na salama pa kuishi kwa kizazi hiki na vizazi vijavyo na kuwawezesha mamilioni ya watu kufikia malengo yao kimaisha.

Uchukuzi SC yawa ya tatu, kipa adaka penati 3

Kipa Willium Barton wa Uchukuzi SC akikaa tayari kupangua penati ya kipa mwenzake wa Tanesco Hashim Yahya. Uchukuzi ilitwaa ushindi wa tatu kwa penati 3-2.

Mchango wa Ndg. Zitto Kabwe Bungeni 28 Aprili 2016.......Kazirudisha Upya hizi Tuhuma mbili za Rushwa

Mheshimiwa Spika, Tangu tuanze Mkutano huu wa Bajeti mwaka 2016 kumekuwa na malalamiko kutoka kwa Wabunge na hasa wabunge wa kambi ya Upinzani Bungeni kuhusu ukiukwaji wa Sheria mbalimbali za nchi katika masuala ya Bajeti. 

DC Wa Kinondoni Ally Hapi Aanza Mapambano Dhidi Ya Watumishi Hewa, Abaini 89 Waliolipwa Zadi Ya Sh Bilioni 1.331


Mkuu  wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi amesema idadi ya watumishi hewa katika wilaya hiyo, imeongezeka hadi kufikia 89 wakiwa wamesababisha hasara ya zaidi ya Sh bilioni moja.

Huduma Ya Treni Ya Abiria Kutoka Dar Kwenda Bara Kuanza Tena Jumapili Mei Mosi, 2016

Treni ya kwanza ya abiria ya Deluxe  kutoka Dar es Salaam kwenda bara itaondoka saa 2 asubuhi siku Jumapili Mei Mosi, 2016 kuelekea Kigoma.

Waziri wa Afya Afunga Mkutano wa Chama cha Maofisa Kumbukumbu na Taarifa za Afya Dar.

Mkurugenzi wa Uhakiki Ubora wa Huduma za Afya kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Mohamed A. Mohamed aliyemwakilisha waziri wa wizara hiyo, akifunga rasmi Mkutano wa Chama cha Maofisa Kumbukumbu na Taarifa za Afya Tanzania (THERIA) leo jijini Dar es Salaam.

UONGOZI WA WANAFUNZI WA CHUO CHA UONGOZI WA FEDHA ZANZIBAR (ZIFASO) WACHAGUA VIONGOZI WAPYA.

z1Wagombea  wa nafasi  ya Rais wa ZIFASO Juma Shirazi Hassan a Makamu wake Zuwena Jaku Hassan (wa katikati) wakiongozwa kuingia katika kampasi ya Chuo cha Uongozi wa Fedha Zanzibar kiliopo Chwaka Mkoa Kusini Unguja tayari kwa ajili ya kupiga kura.

Supastaa wa Malawi Tay Grin awapania Diamond na Vanessa.

unnamed
Rapper na supastaa wa Malawi, Tay Grin, amedai kuwa ana mpango wa kuwashirikisha Diamond Platnumz na Vanessa Mdee. Tay ambaye hivi karibuni aliachia video ya wimbo

Serikali Yashauriwa Kuwa na Hisa Kwenye Kampuni za Madini ili Kujua Mapato halisi Yanayoingizwa na Wawekezaji wa Kigeni.

Serikali imeshauriwa kuwa na sehemu ya umiliki katika kampuni zinazochimba madini na gesi ili kujua mapato halisi yanayoingizwa na wawekezaji wa kigeni. 

Rais Magufuli Aombwa Kuteketeza Meno ya Tembo yaliyohifadhiwa Ghalani


Wanahalakati wa Okoa Tembo wa Tanzania wamemshauri Rais John Magufuli kuteketeza shehena ya meno ya tembo yaliyohifadhiwa ghalani ili kuepuka gharama za uhifadhi na ulinzi.

Donald Trump Ashindwa Kutamka Jina la Tanzania..Ashutumiwa Kuwa na Ufahamu Mdogo wa Diplomasia ya Kimataifa

Mgombea wa urais kupitia chama cha Republican nchini Marekani ambaye amekuwa akiongoza kwenye kinyang’anyiro hicho, Donald Trump amejikuta akikosolewa vikali kuhusu upeo wake juu ya sera za nje pale aliposhindwa kulitamka bayana jina la Tanzania.

Ni kweli Diamond na Zari Wanataka Kuachana? Ni kweli Diamond Kahamishia Majeshi kwa Mrembo Lyn?

Kinachoendelea sahizi instagram ni Mtifuano na ukorochoaji wa Maisha ya watu! Watu wapo busy,watu wapo katika pirika pirika za kutafuta ukweli kujua nini kinacho endelea kati ya Zari na Diamond na Diamond na Video queen wa Kwetu' Mama Diamond na mkwe wake na mawifi mtu!

TID Afunguka 'Nilikuwa Natoka na Wema Sepetu Alafu Akaniambia Hanitaki..Sasa Hivi Akitaka Kurudi Hakuna Nafasi Tena'

Akiwa Katika Kipindi cha Clouds 360 leo Mwanamuziki TID Amefunguka Kuhusu Kutoka na Wema Sepetu...

Mh Mbunge Sugu Amnunulia Mpenzi Wake Gari Mpya Aina ya Lexus..Yazua Gumzo Mtandaoni.

Ripoti kutoka mitandaoni zinasema kuwa Muheshimiwa Mbunge Sugu Amemzawadia Gari aiana ya Toyota Lexus kama zawadi ya siku ya kuzaliwa kwa mpenzi wake ajulikanae kama Happiness,

Mrembo Jack Wolper Afunguka Sababu za Kuacha Kuvaa Nguo za Kiume.


Akiongea kwenye kipindi cha Nirvana, kinachoruka kupitia EATV, Wolper alisema ‘nilikuwa navaa vile kutokana na wakati ule, sasa hivi nimeshakuwa na mchumba’.

WANANCHI JIJINI MBEYA WAJITOKEZA KUPATIWA DAWA ZA KINGA TIBA KWA MAGONJWA YALIYOKUWA HAYAPEWI KIPAUMBELE

Mkuu wa wilaya ya Mbeya Nyilembe Munasa akitoa Dawa za kinga tiba kwa magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele kwa wananchi wa Jiji la Mbeya katika eneo la kituo cha Mabasi madogo(Daladala)Kabwe April 29 -2015 mara baada ya kuzindua rasmi .

DICOTA 2016 YAANZA KWA MCHAPALO WA NGUVU.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania Seattle, WA, Bwn. Mutta (kushoto) akiwa na mkewe wakiangalia majina yao huku Bi. Asha Nyang'anyi (kulia) akijaribu kuwahudumia.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Ijumaa ya April 29

Picha 9 za Jeshi letu la JWTZ Likiwa Katika Uwanja wa Mapambano Huko Congo DRC.

Hapa  kuna Picha Kadhaa za Wanajeshi wetu wa JWTZ  Wakiwa  katika  uwanja wa Mapambano katika Misitu ya Ben Congo DRC.