Kocha
Stewart Hall wa Azam FC ‘amenunua’ ugomvi wa Yanga na Coastal Union kwa
kusema kuwa kuna kila sababu ya kujifikiria mara mbili kwa nini kila
siku itajwe Yanga katika matokeo tatanishi na kuongeza kuwa Yanga
haikupata ushindi halali kutinga fainali ya Kombe la Shirikisho.
Mchezo
wa Yanga na Coastal ulivunjika katika dakika 15 za mwisho za nyongeza
ambapo Yanga ilikuwa ikiongoza mabao 2-1, baada ya kupitia ripoti ya
mchezo, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) likaipa Yanga ushindi kwa
madai kuwa mashabiki wa Coastal walikuwa chanzo cha mchezo huo
kuvunjika.
“Kila
mtu, kila kona hapa gumzo ni mchezo huo wa Coastal na Yanga, hata
katika mitandao ya kijamii na Youtube yanayozungumzwa sana kuhusu soka
la Tanzania ni hujuma, limejaa viashiria vya rushwa,” alisema Hall na
kuongeza:
“Niliona
mchezo ule, bila kificho mabao yote hayakuwa halali, bao la kwanza
aliotea (Donald Ngoma), bao la pili wazi kabisa lilikuwa la mkono,
lakini mwamuzi hakuwa na maamuzi. TFF wanatakiwa kufunguliwa mashtaka.
“Nimekuwa hapa mwaka wa sita sasa, soka linatawaliwa na rushwa lakini kwa sasa imezidi kiwango.”
No comments:
Post a Comment