Kipa
Willium Barton wa Uchukuzi SC akikaa tayari kupangua penati ya kipa
mwenzake wa Tanesco Hashim Yahya. Uchukuzi ilitwaa ushindi wa tatu kwa
penati 3-2.
wa michezo mbalimbali wa timu ya Uchukuzi SC wakishangilia baada ya
timu ya soka kutwaa ushindi wa tatu kwa penati 3-2 dhidi ya Tanesco.
Omary
Kitambo (4) wa Uchukuzi SC akiwania mpira uliopigwa na Stanley Uhagile
wa Tanesco. Uchukuzi ilitwaa ushindi wa tatu kwa penati 3-2.
- Kamba wanaume watwaa ubingwa
Na Mwandishi Wetu, Dodoma
TIMU ya soka ya Uchukuzi SC jana
ilitwaa ushindi wa tatu wa mashindano ya Mei Mosi, baada ya kuwashinda
Tanesco magoli 3-2 kwa mikwaju ya penati, katika mchezo uliofanyika
kwenye uwanja wa Jamhuri mkoani hapa.
Ushindi wa Uchukuzi SC
ulichagizwa na kipa wao mahiri William Barton aliyeweza kudaka penati
tatu kati ya tano zilizopigwa na Tanesco.
Baada ya ushindi huo, Barton
alimwaga machozi ya furaha, kwani alidaka penati zilizopigwa na kipa
mwenzake Hashim Yahya, Khalifa Shekuwe na Abdallah Magubile.
Penati za Uchukuzi SC zilifungwa
kwa ufundi stadi na Fidelis Kyangu, Masoud Masoud na Kado Nyoni, wakati
waliokosa ni Omary Said ‘Chidi’ na Seleman Kaitaba.
Hatua ya penati ilifuatiwa baada
ya timu hizo kutoka suluhu katika dakika 90 za kawaida na kwa mujibu wa
sheria za mashindano hayo hakina nyongeza ya dakika 30 na inapigwa
mikwaju ya penati moja kwa moja.
Kocha wa Uchukuzi SC, Elutery
Muholeli alisema kuwa mchezo ulikuwa na ushindani mkubwa, na wachezaji
wake walicheza kwa kujituma, na dhamira yao ilikuwa ni kutwaa ubingwa,
lakini bahati haikuwa yao na wamebahatika kutwaa ushindi wa tatu.
Naye kocha wa Tanesco, James
Washokera alikiri wachezaji wake kukosa umakini kutokana na kikosi chake
kukosa wafungaji, na aliamua kuwatumia viungo zaidi, ili kufunga magoli
lakini walishindwa kutokana na kucheza nafasi sio yao.
“Unajua hii timu yetu ilitakiwa
kuwa ni kombaini ya Tanesco Tanzania nzima, lakini haikuwa hivyo na
badala yake wametoka sehemu chache na nilitarajia ningechagua wafungaji
kutoka mikoani, lakini sikupata nafasi hiyo, ila hili tatizo huu ndio
mwisho wake na mwakani tutakuja kamili kwani nitahakikisha ninazunguka
na kupata wachezaji sehemu zote,” alisema Washokera.
Pia Uchukuzi wanaume wameibuka
mabingwa wa mchezo wa kamba baada ya kumaliza ikiwa imejikusanyia pointi
10, na haikuwahi kuvutwa na timu yeyote tangu michuano hiyo ianze.
Nayo CDA ‘Watoto wa nyumbani’
wameshika nafasi ya tatu katika mchezo wa netiboli wakiwa na pointi tatu
sawa na Tanesco iliyoshika nafasi ya nne , lakini wanatofautiana kwa
magoli ya kufunga na kufungwa, huku TPDC ikiburuza mkia ikiwa haijapata
pointi yeyote.
No comments:
Post a Comment