Friday, 29 April 2016

HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI-MNH- YAMEKA MIKAKATI KUHAKIKISHA WATOTO WANAOZALIWA NA MATATIZO YA KUTOSIKIA WANAPATIA MATIBABU.

wa masikio Fayaz Jaffer akitoa elimu kwa wazazi / walezi , jinsi ya kutunza kifaa kinachomsaidia mtoto mwenye matatizo ya kusikia kuweza kusikia na kuwasiliana. Mtaalam huyo ametoa elimu hiyo leo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili-MNH- alipokuatana na wazazi ambao watoto wao walifanyiwa upasuaji nchini India na kuwekewa kifaa hicho.

C2 
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili –MNH- Profesa Lawrence Museru akielezea mipango ya MNH katika kuhakikisha huduma hiyo inakuja kutolewa hapa MNH kwa siku zijazo

C5 
Baadhi ya wazazi wakimsikiliza mtaalam wa Masikio Fayaz Jaffer leo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili-MNH.
C3 
Kaimu Mkurugenzi wa MNH Profesa Lawrence Museru pamoja na Mtaala wa masikio Fayaz Jaffer wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watoto ambao walifanyiwa upasuaji na kuwekewa kifaa maalum cha kuwasaidia kusikia ili kuweza kuwasiliana.
C4 
Kaimu Mkurugenzi wa MNH Profesa Museru ( katikati) akiwa na Mkuu wa Idara ya Masikio , Pua na Koo Daktari Edwin Liyombo ( kushoto ) na Fayaz Jaffer .

Hospitali ya Taifa Muhimbili-MNH- imeweka mikakati ya kuhakikisha watoto wanaozaliwa na matatizo ya kutosikia wanapatia matibabu hayo katika Hospitali hiyo ili kuwawezesha watoto wengi wenye matatizo hayo kupata huduma hiyo kwa wakati.
Mikakati hiyo imeelezwa leo jijini Dar es salaam na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa MNH Profesa Lawrence Museru wakati akizungumza na wazazi / walezi ambao walifika MNH kwa ajili ya kufuatilia maendeleo ya watoto wao ambao wana matatizo ya kusikia sanjari na kupata maoni mbalimbali kutoka kwa wazazi hao.
Akifafanua Profesa Museru amesema kimsingi mahitaji ya matibabu hayo ni makubwa na upasuaji huo haufanyiki nchini  hivyo wagonjwa hutegemea matibabu hayo nje ya nchi na ambayo ni gharma kubwa .
“ Mpango uliopo sasa ni kuhakikisha huduma hiii inafika hapa MNH ili wagonjwa wenye matatizo hayo waweze kutibiwa hapa nchini kwasababu tuna wataalam wa kutosha , pia naamini hatua hiyo itawasaidaia wananchi wengi kupata  matibabu hayo ” amesema Profesa Museru.
Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Masikio ,Pua na Koo wa MNH  Daktari Edwin Liyombo amesema tayari dokezo limeandaliwa ili kuiomba serikali kuanzisha program maalum itakayowasaidia Madaktari kupata mafunzo pamoja na kupata vifaa tiba ili upasuaji huo uweze kufanyika hapa nchini.
Kwa  mujibu wa Daktari Liyombo mgonjwa mmoja akipelekwa nchini India kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji hugharimu kati ya Shilingi Milioni 85 hadi Milioni 100  lakini endapo matibabu hayo yatafanyika hapa nchini gharama itapungua kwa kiasi kikubwa.
Akizungumzia kuhusu utaratibu wa kukutana na wazazi  ambao watoto wao wana matatizo ya kusikia, Daktari Liyombo amesema utaratibu huo ni endelevu kwani una lenga kufuatilia maendeleo ya mtoto na kumuwezesha mzazi kupata ushauri wa kitaalam , leo zaidi ya wazazi 40 wamejitokeza MNH kwa ajili ya kukutana na watalaam

No comments: