Monday, 2 May 2016

WAMBURA-SITAKUBALI RASILIMALI ZA TAIFA HILI ZICHEZEWE.

a1
Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe Anastazia Wambura(wa pili kushoto) akipata msaada wakati akiteremka toka katika kiwanja cha shirika la utangazaji Tanzania(TBC) kulipojengwa nyumba za watumishi wa shirika hilo ambazo hazijaisha kwa zaidi ya miaka 20 sasa na kutoa maagizo ya kumalizia nyumba hizo au kuwapa Halmashauri ya Kisarawe ili wajenge Hostel za wanafunzi.(Picha na Daudi Manongi-WHUSM)

a2
Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu wa shirika la utangazaji Tanzania(TBC) Bi.Joselin Lugola akitoa mrejesho kuhusu nyumba za shirika hilo zilizo kisarawe mkoani Pwani ikiwemo kukamilisha upatikanaji wa hati  wa eneo hilo na kuliendeleza ili watumishi wa TBC wa kisarawe walitumie kwa makazi.

a3
Kaimu mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Bi.Nahya Mansour(wa kwanza kushoto) akimskiliza Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe Anastazia Wambura(hayupo pichani) wakati akitoa maagizo juu ya nyumba za Shirika la Utangazaji Tanzania(TBC) zilizopo eneo la kimani Kisarawe mkoa wa  Pwani.wengine pichani ni Mkurugenzi mtendaji wilaya ya Kisarawe Bi.Mwanamvua Mrindoko(wa pili kushoto).

a4
Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe Anastazia Wambura akitoa maelekezo kwa Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu wa shirika la utangazaji Tanzania(TBC) Bi.Joselin Lugola wakati alipofanya ziara katika nyumba za shirika hilo zilizopo kisarawe mkoani Pwani.

Naibu Waziri Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Anastazia Wambura ametoa wito kwa Shirika la Utangazaji Tanzania(TBC) kutunza Rasilimali za Taifa kwa kuwa ni pesa inayotoka na jasho la mlipa Kodi na ingeweza kutumika kwa kazi nyingine kuliko uharibifu unaofanyika katika kiwanja cha Shirika hilo kilicho eneo la kimani ambako zimejengwa nyumba za wafanyakazi wa shirika hilo waliopo kisarawe mkoa wa Pwani.
Mhe.Wambura alisema hayo wakati alipotembelea eneo la shirika hilo ili kupata mrejesho wa maagizo aliyotoa wakati alipofanya ziara ya kwanza katika eneo hilo Aprili 2011 mwaka huu na kuipatia siku saba Idara ya Miradi ya shirika hilo ikishirikiana na Halmashauri ya kisarawe kufanikisha upatikanaji wa hati miliki ya eneo hilo la makazi ya wafanyakazi wa shirika hilo.
“Taratibu za Kisarawe za upatikanaji wa hati zimekamilika na sasa wamepeleka ile Rasimu kwa kamishna wa hati kanda ya mashariki ,na maelezo tumeyaskia kwamba kulikuwa na kupishana katika uaandaaji wa hati ndo maana ikachelewa lakini kwa sasa hivi bado tunaitaji kulinda rasilimali za Taifa.Tunaitaji kuzuia uhalibifu”,Alisema Mhe Wambura.
Aidha Mhe Wambura ametoa maagizo kwa shirika hilo kuangalia uwezekano wa kuendeleza makazi hayo kwa kuwa mpaka sasa imepita miaka 20 eneo hilo halijaendelezwa na shirika hilo au kufanyiwa uwekezaji wowote au wakabidhi eneo hilo kwa halmashauri ya kisarawe ili wajenge hostel za wanafunzi na kuongeza kwamba yeye hatakubali eneo hilo lipotee kwa uharibifu kwa wananchi  kubomoa nondo na kuuza kama vyuma chakavu.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu wa Shirika la Utangazaji Tanzania(TBC) Bi.Joselin Lugola alimwahidi waziri huyo kuwa watahakikisha kwenye bajeti ya mwaka 2017/18 suala hilo linashughulikiwa  na kudai kwamba mara nyingi wanaweka pesa ya ukarabati lakini inakatwa lakini wataanza ukarabati kwa awamu kwa mikoa ya Arusha na Mwanza na makao makuu kwa hiyo hata izi za kisarawe zitakarabatiwa mara moja.

No comments: