Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais
anayeshughulikia Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, George
Simbachawene amesema mradi wa Mabasi Yaendayo Kasi (Dart), unatarajia
kuanza rasmi Mei 10, mwaka huu.
Akizungumza kwenye majumuisho ya ziara
ya Kamati ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa, Simbachawene alisema
baada ya kukutana na wadau wa mradi huo, wamewahakikishia kuwa utaanza
rasmi mwezi ujao bila kukosa.
“Tumeambiwa mradi huu una mikataba mingi
na kuwa bado kuna mjadala mkubwa wa mikataba. Hatuwezi kulazimisha maana
unaweza kujikuta ukitengeneza mikataba mibaya, hivyo tunaendelea na
mijadala ya mikataba,” alisema.
Mwenyekiti wa kamati hiyo, Jasson
Rweikiza alisema wameutembelea mradi huo zaidi ya mara nne na kugundua
tatizo linaloukwamisha kuwa ni fedha na kuitaka Serikali kutoa fedha
ili uanze.
Aliesema lengo la kuanzishwa kwa mradi huo ni kupunguza kero
ya usafiri kwa wakazi wa Jiji la Dar es Salaam wanaokabiliwa na tatizo
la usafiri na foleni za barabarani, hivyo kutumia muda mrefu barabarani.
No comments:
Post a Comment