Utafiti uliofanyika hivi karibuni na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS)
umebaini kwamba asilimia 71 ya watanzania wanatumia muda mwingi kufanya
shughuli zisizokuwa za uzalishaji mali wala tija binafsi kwao na kwa
Taifa kwa ujumla.
Akizundua taarifa ya utafiti huo leo jijini Dar es salaam Waziri wa Nchi
Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye
ulemavu Mhe. Jenista Mhagama amesema kuwa idadi hiyo hufanya kazi
zisizoleta tija kwao na taifa na muda mwingi huutumia kujihudumia
binafsi kwa kulala na starehe nyingine.
Ameeleza kuwa takwimu hizo zinaonesha wazi ni kwa namna gani watanzania
wanashindwa kujishughulisha katika kufanya kazi zenye kuwaingizia kipato
na badala yake wanatumia muda wao mwingi kufanya shughuli zisizo za
uzalishaji hasa kufanya starehe mbalimbali.
“Ndugu zangu watanzania unakuta mtu amekaa baa au anacheza “poll table”
kuanzia asubuhi mpaka jioni na hujui anafanya kazi gani ya uzalishaji,
ndugu zangu tuone aibu basi tujishugulishe tulijenge taifa letu ili
kujiletea maendeleo yetu na nchi yetu.”
Aidha, matokeo hayo yamebainisha kuwa asilimia 18.5 ya wananchi
wanafanya kazi za uzalishaji na asilimia 10.6 ni wale wanaofanya
shughuli za nyumbani zisizo na malipo huku uchambuzi wa kijinsia
ukionesha kuwa wanaume asilimia 23.8, wanatumia muda mwingi kwenye
shughuli za kiuchumi ikilinganishwa na asilimia 13.5 ya wanawake.
No comments:
Post a Comment