Timu ya Leicester City imeshinda ubingwa wa Ligi Kuu ya Uingereza kwa mara ya kwanza na kuweka historia kubwa ya mchezo wa soka nchini humo.
Ushindi huo umetokana na Tottenham kutoa sare ya magoli 2-2 na Chelsea jana usiku, na kusaidia kuipatia mafanikio timu hiyo inayonolewa na kocha Claudio Ranieri.
Leicester City ilianza kampeni ya kuwania taji hilo katika msimu huu kwa mafanikio baada ya kunusurika kushuka daraja katika msimu uliopita.
Mashabiki wa Leicester City wakishangilia ubingwa baada ya Chelsea kutoa sare na Tottenham
Eden Hazard akipiga mpira uliozaa goli la kusawazisha la Chelsea
Mpira uliopigwa na Eden Hazard ukitinga wavuni huku kipa wa Tottenham akishindwa kuuzuia.
No comments:
Post a Comment