Monday, 11 April 2016

Darfur kupiga kura ya maoni leo


Image capti
Kura ya maoni itaamua kama Darfur itakuwa na majimbo matano au jimbo moja, ambapo raia watakuwa na siku mpaka ya jumatano kuamua.

Kura hii inapigwa wakati kukiwa na hali duni ya usalama na watu wengi hawajajiandikisha kupiga kura.
Marekani imeeleza hofu yake kuwa kura hiyo haitakuwa ya haki, lakini Rais Omar al-Bashir amesisitiza kuwa itakuwa huru na haki.
Kura ya maoni ni hatua ya mwisho ya mchakato wa kuleta amani ambayo makubaliano yake yalitiwa saini mjini Doha kwa kipindi kirefu waasi wamekuwa wakiomba kuwepo na mamlaka kwenye miji ili kuzuia kile wanachodai kuingilia kwa mamlaka ya Khartoum kwenye mizozo ya umiliki wa ardhi.

No comments: