Monday, 11 April 2016

RAIS DKT. MAGUFULI APOKEA TAARIFA YA MWAKA YA UTENDAJI WA TAASISI YA TAKUKURU PAMOJA NA HUNDI KIFANI YA SH. BILIONI 6 KUTOKA BUNGE BAADA YA KUBANA MATUMIZI.


MLO1
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Taarifa ya Mwaka ya utendaji wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi hiyo Kamishna Valentino Mlowola Ikulu jijini Dar es Salaam.

MLO2
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Hundi Kifani yenye thamani ya Shilingi Bilioni Sita kutoka kwa Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson mara baada ya Taasisi ya Bunge kutekeleza kwa vitendo kauli ya kubana matumizi yasio na Tija ili fedha hizo zikanunulie madawati kwa ajili ya wanafunzi.
MLO3
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiitazama Hundi Kifani yenye thamani ya Shilingi Bilioni Sita mara baada ya kukabidhiwa na Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson mara baada ya Bunge kutekeleza kwa vitendo kauli ya kubana matumizi ili fedha hizo zikatumike kwa ajili ya ununuzi wa madawati kwa ajili ya wanafunzi.
MLO4
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson kulia, Katibu wa Bunge Dkt. Thomas Kashilillah pamoja na wafanyakazi wengine wa Bunge wakiwa wameishika hundi Kifani hiyo yenye thamani ya Shilingi Bilioni Sita. Rais Dkt. Magufuli ameipongeza Taasisi ya Bunge kutokana na hatua hiyo ya kubana matumizi na kuamua fedha zao zitumike katika kununulia madawati kwa ajili ya wanafunzi.
MLO5
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiwa ameishika Taarifa ya Mwaka ya utendaji wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mara baada ya kukabidhiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi hiyo Kamishna Valentino Mlowola Ikulu jijini Dar es Salaam.
MLO6
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson kabla ya kukabidhiwa hundi kifani yenye thamani ya Shilingi Bilioni Sita.
MLO7
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza katika tukio hilo la upokeaji wa Taarifa yaUtendaji wa  TAKUKURU pamoja na upokeaji wa Hundi Kifani kutoka Taasisi ya Bunge Ikulu jijini Dar es Salaam.
MLO8
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akisisitiza jambo katika Hotuba yake ambayo pia alitengua uteuzi wa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Ane Kilango Malecela ambaye alikubali kutoa taarifa ambazo si sahihi kuwa Mkoa wa Shinyanga hauna watumishi hewa, japo katika uhakiki uliofanyika mara baada ya taarifa hiyo kumebainika kuwa kuna zaidi ya watumishi 45 ambao ni hewa.
MLO9
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Mhandisi John Kijazi  pamoja na Waziri wa Ofisi ya Rais Tamisemi, Utumishi na Utawala bora Angela Kairuki Ikulu jijini Dar es Salaam.
MLO10
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na  Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi John Kijazi wapili kulia, Dkt. Tulia Ackson wakwaza kulia, Katibu wa Bunge Dkt. Thomas Kashilillah  wakwanza kushoto, Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Kamishna Valentino Mlowola Ikulu Jijini Dar es Salaam.
MLO11
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi Katibu Mkuu Kiongozi  Balozi Mhandisi John Kijazi Taarifa ya Mwaka ya utendaji kazi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Ikulu jijini Dar es Salaam.
MLO12
Baadhi ya Viongozi wa juu wa Jeshi la Magereza pamoja na Jeshi la Kujenga Taifa JKT wakisikiliza kwa makini maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli aliyokuwa akiyatoa Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU

No comments: