Msaidizi wa kisheria katika soko la Tabata Muslim, Aisha Juma
akizungumza wakati akifungua tamasha la kuongezea uelewa kuhusu kupinga
ukatili wa kijinsia masokoni lililofanyika mwishoni mwa wiki Soko la
Tabata Muslim jijidi Dar es Salaam ambapo ilielezwa kupungua kwa vitendo
vya ukatili katika soko hilo. Upunguaji wa vitendo hivyo vya ukatili wa
kijinsia umetokana na elimu iliyotolewa na wasaidizi hao wa kisheria
kwa msaada wa Shirika la Equality for Growth (EfG)
Msaidizi
wa kisheria katika soko hilo, Irene Daniel akielezea kupungua kwa
vitendo hivyo vya ukatili wa kijinsia katika soko hilo kutokana na
msaada wa wasaidizi hao wa kisheria masokoni waliowezeshwa na Shirika la
EfG.
Msaidi wa kisheria katika soko hilo akichangia jambo.
Ofisa
Ufuatiliaji na Tathmini wa Shirika la EfG, Mr Shabani akitoa ufafanuzi
wa masuala mbalimbali ya ukatili wa kijinsia masokoni.
Wasanii
wa Kundi la Machozi lenye maskani yake Temeke jijini Dar es Salaam
wakitoa burudani kwenye tamasha hilo lililofanyika mwishoni mwa wiki
viwanja vya Soko la Tabata Muslim.
No comments:
Post a Comment