George Fellowes ni mwanafunzi wa chuo kikuu mwenye umri wa miaka 22 na anaamni kwamba hata yeye hupatwa na ''hedhi ya kiume''.
Anasema
kuwa ni rafiki wa karibu wa Amber May Ellis jirani yake na hivyobasi
hupata uchungu wa hedhi kila mwezi rafikiye anapopata hedhi.
Uchungu
huo anasema huwa mkali hadi kulazimika kuchukua likizo ya kuwa
mgonjwa.Akizungumza na Newsbeat,George anaelezea:Nadhani ni swala la
kifikra kwa sababu sisi ni marafiki wa karibu sana na tuna hisia sawa.
Katika
kipindi cha miaka mitatu iliopita anasema kuwa amekuwa akipata uchungu
wa hedhi na ishara hizo ni sawa na zile za wanawake.
Ninapata
uchungu chini ya tumbo langu pamoja na katika kinena.Huwa nahisi vibaya
na kuwa na hasira na marafiki wangu wengi.Pia huwa na hisia zenye
mhemuko.
''Huwa sipendi kulia wakati huo lakini huwa na hasira nyingi.Kuna kitu kimoja kisichomuathiri George hatahivyo.
Sidhani kwamba wanaume wanaweza kupata hedhi bila kutokwa na damu'',anasema.
''Wakati unapokuwa rafiki wa karibu na mtu nadhani homoni zenu hufanana''. |
No comments:
Post a Comment