Wateja wengi wamefika katika matawi ya benki hiyo wakitaka kutoa pesa zao
Benki moja nchini Kenya imewekwa chini ya mrasimu baada ya wateja
kutoa pesa zao kwa wingi kufuatia wasiwasi kuhusu uthabiti wa benki
hiyo.
Wengi wa wateja wamefika kwa wingi katika mashine za kutolea fedha (ATM) leo lakini wakapata mashine hizo zimefungwa.
Benki Kuu ya Kenya (CBK), taasisi iliyo na jukumu la kusimamia huduma za
benki Kenya, imeamua kuweka benki hiyo ya Chase Bank chini ya mrasimu
ikisema benki hiyo ilishindwa "kutimiza masharti yake kifedha tarehe 6
Aprili”.
CBK imesema hatua hiyo imechukuliwa kwa maslahi ya „walioweka pesa kwenye benki hiyo, wanaoidai pesa benki hiyo na umma.”
Benki hiyo sasa itasimamiwa na shirika la Kenya Deposit Insurance Corporation (KDIC).
Gavana wa CBK Dkt Patrick Njoroge ameambia wanahabari kwamba Chase Bank
haikuweza kutimiza mahitaji ya kimsingi kama vile „kuhamisha pesa za
wateja”.
Matawi yote 62 ya benki hiyo nchini Kenya yalifungwa jioni, Dkt Njoroge
akisema hatua hiyo ilitumiwa kuilinda benki hiyo baada ya wateja wengi
kujitokeza kutoa pesa. |
No comments:
Post a Comment