Thursday, 7 April 2016

Haya ndio yaliyo ajili sudani kusini Riek Machar kurudi Juba kwa wadhfa mpya.


 Riek Machar

Kiongozi wa upinzani nchini Sudan Kusini Riek Machar amethibitisha kwamba atarudi katika mji mkuu wa taifa hilo Juba mnamo mwezi Aprili tarehe 18.
Bw Machar anatarajiwa kuchukua wadhfa wa makamu wa rais katika serikali ya muungano iliobuniwa na mkataba wa amani unaolenga kumaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyoanza mwezi Disemba mwaka 2013.

Mapigano kati ya waasi wa bw Machar na wanajeshi wa serikali ya rais Salva Kiir yamesababisha zaidi ya watu milioni 2 kukosa makao katika taifa hilo changa duniani.


Salva Kiir na Riek Machar

Katika barua kwa mkuu wa bodi inayochunguza makubaliano hayo ya amani Bw Machar amesema kuwa atabuni yeye pamoja na rais Salva Kiir serikali ya mpito na kuanzisha baraza la mawaziri wa serikali ya mpito.
Kumekuwa na wasiwasi kuhusu kucheleweshwa kuidhinishwa kwa mkataba huo uliotiwa saini mwezi Agosti.

No comments: