Mwanamuziki wa dance, Ndanda Kosovo aliyefariki wikiendi iliyopita, atazikwa leo kwenye makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Muda mfupi uliopita mwili wake uliwasili kutoka Muhimbili ulikokuwa umehifadhiwa tayari kwa shughuli za kutoa heshima za mwisho.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo, Nape Nnauye atawaongoza watu waliohudhuria msiba huo kwenye mazishi.
Ndanda aliyewika na kundi la FM Academia Wajelajela, alikuwa akisumbuliwa na tatizo la tumbo ambapo inadaiwa kuwa mshipa mmojawapo tumboni ulipasuka hali iliyompelekea kuwa anatapika tamu.
Tazama picha zaidi hapo chini.
No comments:
Post a Comment