Mratibu wa Heart Marathon Dkt. Omary
Chillo (katikati) akiongea na waandishi wa habari kuhusu mashindano ya
mbio maalum za kupambana na ongezeko la magonjwa yasiyoambukiza
zijulikanazo kama Heart Marathoni zinazotarajiwa kufanyika Aprili 26
mwaka huu jijini Dar es salaam, kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Kamati
ya maandalizi ya Heart Marathon Dkt. Chaka Halfani na kulia kwake ni
Kaimu Katibu Chama cha Riadha Tanzania Bi.Ombeni Zavala.
Mratibu wa Heart Marathon Dkt. Omary Chillo (wa kwanza
kulia) akiongea na waandishi wa habari kuhusu mashindano ya mbio maalum
za kupambana na ongezeko la magonjwa yasiyoambukiza zijulikanazo kama
Heart Marathoni zinazotarajiwa kufanyika Aprili 26 mwaka huu jijini Dar
es salaam, kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya Heart
Marathon Dkt. Chaka Halfani na Mratibu Msaidizi Heart Marathon
Bi.Catherine ikangaa.
4 Mwenyekiti wa Kamati ya
maandalizi ya Heart Marathon Dkt. Chaka Halfani akionyesha kwa
waandishi wa habari namba watakazopewa washiriki wa mbio maalum za
kupambana na ongezeko la magonjwa yasiyoambukiza zijulikanazo kama Heart
Marathoni zinazotarajiwa kufanyika Aprili 26 mwaka huu jijini Dar es
salaam,kulia kwake ni.Mratibu wa Heart Marathon Dkt. Omary Chillo na
Kaimu Katibu Chama cha Riadha Tanzania Bi.Ombeni Zavala .
Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya Heart Marathon Dkt.
Chaka Halfani akionyesha kwa waandishi wa habari fulana watakazovaa
washiriki wa mbio maalum za kupambana na ongezeko la magonjwa
yasiyoambukiza zijulikanazo kama Heart Marathoni zinazotarajiwa
kufanyika Aprili 26 mwaka huu jijini Dar es salaam,kulia kwake
ni.Mratibu wa Heart Marathon Dkt. Omary Chillo.
Taasisi ya Tanzania Health
Summit imeandaa mbio maalumu za kupambana na ongezeko la magonjwa
yasioambukiza yajulikanayo kama Heart Marathon zitakazofanyika Aprili
26, 2016 katika viwanjwa vya michezo vya Chuo Kikuu jijini Dar es
salaam.
Hayo yamesemwa na Mratibu
Kamati ya Maandalizi ya Mbio hizo Dkt. Omary Chillo ambapo amesema kuwa
lengo lake ni kusaidia juhudi za Serikali na wadau wa Sekta ya Afya
kupunguza tatizo linalokuwa kwa kasi la magonjwa yasioambukizwa hapa
nchini.
“Watanzania wote kwa ujumla
tunawaalika kushiriki katika mbio za Heart Marathon zitakazoambatana na
upimaji wa magonjwa yasiyoambukizwa na kutoa ushauri wa kitaalamu kwa
ugonjwa wa Kisukari, Shinikizo la Damu, Uwiano wa urefu na uzito, wingi
wa mafuta mwilini pamoja na Saratani ya matiti” alisema Dkt. Chillo.
Amesema mbio hizo zinatarajiwa
kuwa na washiriki zaidi ya 2,000 kutoka taasisi, makampuni, mashirika,
familia na jamii kwa ujumla, rika tofauti ikiwemo watoto, vijana na
wazee, makundi ya walemavu na watu wenye magonjwa yasioambukiza
watashiriki.
Aidha, Dkt. Chillo ameongeza
kuwa mbio hizo zimegawanywa kwa umbali tofauti ambazo ni mbio ndefu za
Kilometa 21.1 kwa ajili ya wakimbiaji wazoefu, kilometa 10 kwa
wakimbiaji wa kati, Kilometa 5 wakimbiaji wa kawaida, kifamilia na
kampuni pamoja na mbio za watoto chini ya miaka 12 watakimbia umbali wa
mita 700.
Kauli mbiu kwa mwaka huu katika mbio maalumu za kupambana na ongezeko la magonjwa hayo ni “Epuka magonjwa yasioambukiza”
Viingilio katika mbio hizo
maalumu zitakuwa kuanzia elfu tano kwa watoto wa chini ya umri wa mika
13 hadi Shilingi 10,000 kwa mtu mmoja ambapo watu wenye ulemavu
hawatalipia kiingilio.
No comments:
Post a Comment