Mtaalam
wa Jiografia kutoka Chuo Kikuu Ardhi Dkt. Mlenge Fanuel Mgendi
akiwahamasisha wanafunzi wa kidato cha Sita wa Shule ya Sekondari ya
Wasichana ya Jangwani kupenda kusoma na kuweka bidii katika masomo
ambayo wanauwezo nayo ili yawasaidie kuendelea na Elimu ya Juu katika
chuo Kikuu Ardhi leo jijini Dar es salaam. Chuo Kikuu Ardhi kinaendesha
Programu ya utoaji elimu kwa wanafunzi wa sekondari katika shule
mbalimbali kwa lengo la kuwasaidia kufanya uchaguzi sahihi wa kozi za
masomo wanazotarajia kuendelea nazo pindi watakapohitimu masomo ya elimu
ya Sekondari.
Mwanataaluma
wa Chuo Kikuu Ardhi Bi. Latifa Litwe (kushoto) akitoa elimu kwa
wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Jangwani namna ambavyo
Chuo Kikuu Ardhi kinawajengea uwezo kielimu wanafunzi wanaosoma katika
chuo hicho kukabiliana na mabadiliko ya Tabia Nchi na majanga mbalimbali
pamoja na ushauri kuhusu sekta ya Ardhi kwa ujumla hapa nchini ikiwemo
uhifadhi wa Ardhi na Sayansi ya Udongo.
Baadhi
ya wanafunzi wa Kidato cha Sita wa Shule ya Wasichana ya Jangwani
wakiangalia na kufurahishwa na moja ya Kazi ya Ubunifu wa Majengo na
mitaa iliyofanywa na wanafunzi wa Chuo Kikuu Ardhi mwaka wan nne leo
jijini Dar es salaam.
Mwanataaluma
wa Chuo Kikuu Ardhi Bw. Dennis Tesha akiwaeleke za wanafunzi wa shule
ya wasichana ya Jangwani namna bora kuchagua masomo yao ya baadaye
kulingana na sifa walizonazo watakapotaka kujiunga na vyuo vikuu hapa
nchini pamoja na kazi watakazofanya mara baada ya kuhitimu kulingana na
masomo yao.
Moja ya kazi ya Ubunifu wa jengo la ghorofa lilobuniwa na mwanafunzi wa Chuo Kikuu Ardhi.
Baadhi
ya wanafunzi wa Kidato cha Sita wa Shule ya Wasichana ya Jangwani
wakifurahia jambo mara baada ya kuangalia moja ya kazi ya ubunifu wa
majengo iliyofanywa na wanafunzi wa mwaka wan ne wa Chuo Kikuu Ardhi
walipokuwa wakizungumza na Afisa Uhusiano wa Chuo hicho Bi. Khadija leo
jijini Dar es salaam.
No comments:
Post a Comment