Wednesday, 13 April 2016

Sakata la AKA Na mapromota Afrika kusini lapiga hatua zaidi.


aka
Watayarishaji wa tamasha kubwa la hiphop la Back to the City nchini Afrika Kusini wameshangazwa na sababu za AKA kukataa kufanya show kwenye tamasha hilo siku chache baada ya kauli kali ya Aka kusamba mitandaoni.

AKA alisema “Sipendezwi na jinsi watayarishaji wa matamasha Afrika kusini wanavyofanya kazi na wasanii wa nyumbani, hata Mimi ni msanii wa kimataifa na nataka kufanyiwa na kuchukuliwa sawa na wasanii wa kigeni mnaowaita wasanii wa kimataifa na ndio maana sitafanya show kwenye Back To The City“.
Aka pia amekata kufanya show hio kutokana na misingi yake kuwa alitaka kutangazwa kama wanavyotangazwa wasanii wa kimataifa wanaokuja kufanya show hio kama Elzhi wa kundi la Slum Village kutoka American.
Pia AKA alitaka show tofauti yenye Bendi, Fataki, mfumo bora wa Taa na muda zaidi wa kufanya show kitu ambacho kimekuwa na mvutano mkubwa kati yake na waandaji wa tamasha hili.

No comments: