Droo
ya Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup)
imefanyika usiku huu moja kwa moja (live) kupitia kituo cha luninga cha
AzamTwo, huku timu za Coastal Union na Mwadui FC zikipata nafasi ya
kucheza nyumbani.
Katika droo hiyo iliyochezeshwa na
mchezaji mstaafu wa timu ya timu ya taifa ya wanawake (Twiga Stars),
Esther Chaburuma, imewashuhudia vigogo wa Ligi Kuu ya Vodacom, Azam FC
na Young Africans wakipata nafasi ya kucheza michezo hiyo katika viwanja
vya ugenini.
Mwadui FC watakua wenyeji wa Azam
FC katika mchezo unaotarajiwa kucheza Aprili 24, 2016 mjini Shinyanga,
huku wagosi wa Kaya Coastal Union wakicheza dhidi ya Young Africans
katika uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga siku hiyo hiyo.
Washindi wa michezo hiyo ya Nusu
Fainali, watakutana fainali ya kombe hilo itakayofanyika mwezi Mei,
ambapo Bingwa wake ataiwakilisha Tanzania katika michuano ya kombe la
Shirikisho barani Afrika (CAF CC).
Wakati huo huo wadhamini wa
michuano hiyo Azamtv kupitia kituo chake cha michezo cha Azam Sports,
leo wameweza kulionyesha hadharani kwa mara ya kwanza kombe la ubingwa
kukikabidhi kwa Katibu Mkuu wa TFF, Mwesigwa Selestine.
No comments:
Post a Comment