TAASISI
ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU)mkoani Pwani imesema
serikali ya mitaa katika mamlaka za watendaji wa vijiji ,mitaa na kata
inaongoza katika vitendo vya rushwa huku wilaya ya Bagamoyo ikielezwa
inaongoza kimkoa .
Aidha idara nyingine zinazoongoza katika vitendo hivyo ni sanjali na idara ya afya,polisi,mahakama,ardhi, sekta binafsi,elimu,tanesco,fedha, vipimo,uhamiaji na maji.
Akitoa
taarifa ya utendaji kazi wa ofisi hiyo kwa kipindi cha miezi mitatu
kuanzia jan hadi march mwaka huu,kwa waandishi wa habari jana,kamanda wa
TAKUKURU mkoani hapo,Suzana Raymond ,alisema walipokea malalamiko 64
kwa kipindi hicho.
Alielezea
kuwa kati ya malalamiko hayo malalamiko 49 yanahusiana na vitendo vya
rushwa na uchunguzi wake unaendelea ambapo 15 kati ya yake hayahusiani
na vitendo vya rushwa.
Kamanda
Suzana alisema idara ya inayoongoza kwa malalamiko ya vitendo hivyo ni
serikali ya mitaa ambayo ina malalamiko 18,ikifuatiwa na afya yenye
malalamiko 8,polisi matano na Mahakama matatu.
Alitaja
upande wa idara ya ardhi imelalamikiwa makosa matatu,sekta binafsi
matatu,elimu mawili,tanesco mawili,fedha moja,vipimo moja,uhamiaji moja
na maji moja.
“Watuhumiwa
hao wengi wao wanalalamikiwa kwa kutumia vibaya mamlaka,kushiriki kuuza
ardhi kinyume na taratibu,kutumia fedha za mapato ya kijiji ,mitaa na
kata kiholel wakati ni matumizi mabaya ya fedha hizo”alielezea Suzana.
Alisema
katika hicho jumla ya kesi mpya nne zilifunguliwa kwenye mahakama za
wilaya na polisi huku kesi 22 zinaenelea kusikilizwa katika mahakama
hizo.
Aidha
kamanda Suzana alieleza kuwa katika kipindi cha july-sept mwaka 2015
kulikuwa na malalamiko ya vitendo vya rushwa 50 na octoba hadi desemba
mwaka huo idadi ya vitendo vya aiina hiyo ilikuwa ni 45.
Hata
hivyo taasisi hiyo mkoani Pwani katika kushughulikia kero za wananchi
kwenye maeneo yanayoongoza kulalamikiwa ni kuendelea kufanya uchambuzi
wa mifumo ili kubaini mianya ya rushwa na kutoa ushauri kwa idara husika
na serikali kwa lengo la kuziba mianya iliyopo.
“Tunaendelea pia kutoa elimu kwa umma kwasasa tumekuwa na utaratibu wa kwenda vijijini kusikiliza kero na malalamiko”
“Kwa
malalamiko ambayo hayahusiani na vitendo vya rushwa tunafikisha katika
idara yenye dhamana pia idara itaendelea kufanya uchunguzi pale ushahidi
utakapopatikana mtuhumiwa ama watuhumiwa watafikishwa mahakamani ili
sheria ichukue mkondo wake”alisema kamanda Suzana.
Akizungumzia
suala la kutoa elimu katika jamii ,Suzana alisema ofisi yao ilielimisha
jumla ya wananchi 4,443 kwa njia ya semina 47 na mikutano ya hadhara
11,kuimarisha klabu za wapinga rushwa 30 katika shule za sekondari na
msingi mkoani humo.
Suzana
alitoa wito kwa jamii kuwa kila mwananchi anapaswa kutambua anao wajibu
wa kupambana na rushwa katika eneo lake kwa kukataa kutoa ama kupokea
rushwa na kuwaomba watoe taarifa kwa taasisi mara wanapobaini kuna mtu
anashiriki vitendo hivyo
No comments:
Post a Comment