Mwili wa Mama Lucy Kibaki, ambaye ni mke wa aliyekuwa rais wa Kenya Mwai Kibaki umewasili leo Jijini Nairobi nchini Kenya ukitokea Uingereza.
Mwili wa Mama Kibaki, umekuja na ndege ya Shirika la Ndege la Kenya KQ, iliyowasili kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta majira ya saa kumi na moja alfajiri.
Katika ndege hiyo pia alikuwemo rais mstaafu Mwai Kibaki na familia yake na marafiki waliokuwa na Mama Kibaki London kwa matibabu na kufariki.
Rais Uhuru Kenyatta na mkewe Margaret walikuwepo uwanja wa ndege kuupokea mwili wa Mama Lucy Kibaki.
Rais mstaafu wa Kenya Mwai Kibaki akishuka kwenye ndege iliyobeba mwili wa mkewe
Rais Uhuru Kenyatta akimpa mkono wa pole rais mstaafu Mwai Kibaki mara tu baada ya kuwasili
No comments:
Post a Comment