Baadhi
ya wadau mbali mbali wa sekta ya usafiri wa anga wakishiriki warsha ya
kujadili rasimu ya Mpango wa Sekta ya Usafiri wa Anga( The Civil
Aviation master Plan) uliofanyika makao makuu ya Mamlaka ya Usafiri wa
Anga Tanzania(TCAA), Banana – Ukonga jijini Dar es Salaam leo.
Wadau wa sekta ya Usafiri wa anga
nchini ,wamekutana katika warsha ya siku moja kujadili rasimu ya mpango
kamambe wa usafiri wa anga yaani ( the Civil Aviation Master Plan)
makao makuu ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga Nchini(TCAA), Banana-Ukonga.
Warsha hiyo iliyowakutanisha
wadau kutoka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, mashirika
yanayotoa huduma za usafiri wa anga nchini , Mamlaka ya Viwaja vya
Ndege na mwenyeji Mamlaka ya Usafiri wa Anga imefunguliwa rasmi na
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Dkt Leonard
Chamuriho.
Lengo la warsha hiyo ni kupata
maoni ya wadau kuhusu rasimu hiyo ya mpango kamambe wa sekta ya usafiri
wa anga nchini ambayo imetayarishwa na kampuni ya LEAPP ya Australia
chini ya udhamini wa Benki ya Dunia. Kampuni hiyo ilianza kuanda rasimu
hiyo mwaka 2015 kazi ambayo imefanyika kwa miezi 12.
Akizungumza wakati wa ufunguzi
huo , katibu Mkuu wa wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano amesema
lengo la serikali ni kuwezesha Tanzania kutoa huduma za usafiri wa
anga kwa mujibu wa viwango na taratibu zinazokubaliwa na Shirika la
Kimataifa la Usafiri wa Anga Duniani (ICAO) pamoja na kuweka mazingira
mazuri yatakayoruhusu ushindani wa kibiashara katika sekta hii.
Ameongeza kuwa sekta ya usafiri wa
anga imekuwa ikikua , mathalani takwimu zinaonyesha safari za ndege
zimeongezeka kwa asilimia 8 katika mwaka 2015 ikilinganishwa na zile
zilizofanyika mwaka 2014. Kadhalika idadi ya abiria imekuwa ikikua kwa
kiwago cha asilimia 1.5- 2 kwa mwaka.
Lengo la warsha hiyo ni kupata
maoni ya wadau kuhusu rasimu hiyo ya mpango kamambe wa sekta ya usafiri
wa anga nchini ambayo imetayarishwa na kampuni ya LEAPP ya Australia
chini ya udhamini wa Benki ya Dunia.
|
No comments:
Post a Comment