Wageni rasmi katika mkutano huo, Wa kwanza kushoto ni Mtafiti kutoka Taasisi ya Mtandao wa Kutathimini Sera za Chakula, Kilimo na Maliasili (FANRPAN), Njongenhle Nyoni, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF), Dkt. Tausi Kida na Mkuu wa Kitengo cha Mazingira kutoka Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Bi. Shakwaanande Natai |
.
Serikali
ya Tanzania kupitia Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi imejipanga
kuhakikisha inawasaidia wakulima kupambana na mabadiliko ya tabia ya
nchi ambayo yanaonekana kuendelea kuikabili nchi.
Hayo
yamesemwa na Mkuu wa Kitengo cha Mazingira kutoka Wizara ya Kilimo,
Mifugo na Uvuvi, Bi. Shakwaanande Natai alipokuwa akizungumza na
waandishi wa habari katika mkutano ulioandaliwa na Taasisi ya Utafiti wa
Uchumi na Jamii (ESRF) na Taasisi ya Mtandao wa Kutathimini Sera za
Chakula, Kilimo na Maliasili (FANRPAN) ili kujadili mpango wa Kilimo
Salama (CSA).
Bi.
Natai alisema serikali inatambua uwepo wa mabadiliko ya Tabia ya Nchi
na kwasasa tayari wataalamu wanafanya tafiti ili waone ni jinsi gani
wanaweza kuwasaidia wakulima kupambana na mabadiliko hayo.
Alisema
kwa sasa bado wakulima wengi hawajafahamu kama kuna mabadiliko ya tabia
ya nchi na hivyo wamekuwa wakitumia njia za asili lakini baada ya
utafiti watapatiwa mbinu mpya za kupambana na mabadiliko ambapo wataweza
kutumia njia za kisasa ambazo zinaonekana kuwa bora zaidi.
“Serikali
inatambua na tunajipanga kuwasaidia wakulima, shida kwa sasa bado
wakulima wengi hawajajua kama kuna mabadiliko ya tabia ya nchi lakini
wataalamu wapo wanafanya tafiti baada ya hapo tutajua tunawasaidia vipi,
“Kwa
sasa kinachoonekana ni kutokueleweka kwa hali ya hewa kama mafuriko
kutokea lakini kwa kuwa bado hawajapatiwa elimu wanashindwa kutambua na
bado wanatumia njia za asili, tutawapa mbinu mpya watafanya kwa pamoja
na mbinu wanazotumia sasa za asili,” alisema Bi. Natai.
Aidha
alieleza kuwa baadhi ya huduma ambazo watapatiwa wakulima baada ya
kukamilika kwa tafiti ni pamoja na kupewa elimu ya kilimo cha
umwagiliaji, mbegu za kisasa ambazo zinawahi kukomaa na dawa za
kupambana na magonjwa.
Nae
mtafiti kutoka FANRPAN, Njongenhle Nyoni alisema taasisi yake imefanya
mkutano huo ili kuona ni jinsi gani wanaweza kupambana na mabadiliko ya
tabia ya nchi katika nchi ambazo wanafanya kazi ambapo Tanzania ni
mojawapo.
Alisema
wao wanafanya tafiti kuona hali ilivyo na baada ya hapo wanatazama
changamoto zilizopo katika kupambana na mabadiliko na wanatoa ushauri ni
jambo gani linaweza kufanyika ili kuwezesha kufanikisha kufanyika
Kilimo Salama (CSA).
“Tunakutana
na watu kutoka asasi za kijamii na taasisi mbalimbali ili kuona ni
jinsi gani CSA inaweza kufanya kazi vizuri hasa katika maeneo tunafanya
nao kazi na hii sio Tanzania tu hata mataifa mengine kama Malawi
tunalifanya hili,” alisema Nyoni.
Pia
iliongeza kuwa malengo ya FANRPAN ni kusaidia wakulima kuondoka katika
janga la umasikini lakini pia kuwepo kwa chakula kilicho katika hali ya
usalama bila kuathiriwa na mabadiliko ya tabia ya nchi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF), Dkt. Tausi Kida akitoa neno la ufunguzi. |
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF), Dkt. Tausi Kida akitoa neno la ufunguzi. |
Mkuu wa Kitengo cha Mazingira kutoka Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Bi. Shakwaanande Natai akielezea Kilimo Salama (CSA). |
Washiriki wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuendelea na mkutano huo.
|
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF), Dkt. Tausi Kida (kushoto) na Mkuu wa Kitengo cha Mazingira kutoka Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Bi. Shakwaanande Natai. |
Karl Deering kutoka Taasisi ya CARE akizungumzia Mpango wa Kilimo Salama Afrika (ACSAA)
|
Baadhi ya wageni katika mkutano huo wakichangia hoja |
Washiriki wa mkutano wakiwa katika makundi kujadili kuhusu Kilimo Salama (CSA)
|
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Uwezeshaji wa ESRF, Doris Likwelile akifunga mkutano
No comments:
Post a Comment