Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetangaza kuwarudishia fedha zao
kesho Jumanne, wapenzi wa mpira wa miguu waliokuwa wameshakata tiketi za
kushuhudia mchezo wa kundi G kati ya Tanzania v Chad jijini Dar es
salaam.
TFF inawaomba washabiki wa mpira wa miguu waliokua wamekata
tiketi za mchezo huo, kufika kesho Jumanne saa 5 kamili asubuhi katika
vituo walivyonunulia wakiwa na tiketi zao ili waweze kurudishiwa fedha
zao.
Zoezi la kuwarudishia fedha
washabiki waliokuwa wameshakata tiketi za mchezo kati ya Tanzania v Chad
litafanyika katika vituo vinne vilivyokua vikiuza tiketi siku ya
Jumapili, hivyo wenye tiketi za mchezo huo wanaombwa kufika na tiketi
zao ili waweza kurudishiwa fedha zao.
Aidha TFF inawaomba radhi watanzania na wapenzi wa mpira wa
miguu kwa usumbufu uliojitokeza na kuwataka kuwa watulivu na wavumilivu
katika kipindi hiki ambacho wanasubiria taarifa zaidi kutoka CAF.
Chad imejiondoa jana katika kinyanganyiro cha kuwania kufuzu kwa
Fainali za Kombe la Mataifa Afrika (AFCON) nchini Gabon mwaka 2017,
ambapo iliku kundi G na timu za Misri, Nigeria pamoja na Tanzania. |
No comments:
Post a Comment