BABA Mzazi wa Mchezaji bora wa Soka bara la Afrika, Ali Samatta (katikati) akiwa na Katibu Mkuu wa Mtandao wa Wasanii Tanzania (SHIWATA) Michael Kagondela kulia na Mhasibu wa mtandao huo, Asha Salvador baada ya kumkabidhi kadi ya uanachama na katiba baada ya kikao cha kuthibitisha mwanae kukubali kupewa ekari tano za kujenga kituo cha wanamichezo, Mkuranga
BABA Mzazi wa Mchezaji bora wa Soka bara la Afrika, Ali Samatta (katikati) akijaza fomu za kukubali masharti ya kujiunga na Mtandao wa Wasanii Tanzania (SHIWATA) mbele ya Mhasibu wa mtandao huo Asha Salvador.
MTANDAO wa Wasanii Tanzania (SHIWATA) umeandaa sherehe za kumkabidhi eneo la kujenga kituo cha michezo mchezaji bora wa Afrika, Mbwana Samatta katika sherehe zitakazofanyika Juni 4, 2016 kwenye kijiji cha Wasani Mwanzega Mkuranga.
Mwenyekiti wa SHIWATA, Cassim Taalib alisema jana Dar es Salaam kuwa maandalizi ya sherehe hizo itaambatana na ugawaji nyumba 31 kati ya hizo moja kubwa, tatu ndogo na misingi 27 ya nyumba hivyo kufikisha jumla ya nyumba 150.
Alisema baba yake Mbwana Mzee Ali Samatta amethibitisha kuwepo kwa mwanae katika sherehe hizo ambazo naye ametunukiwa kuwa mwanachama wa heshima wa mtandao huo na kukubali kushirikiana kuhakikisha michezo inakuwa nchini.
“Baba yake Samatt alisema wakati akiwa kijana alikuwa mfungaji mzuri kwa timu alizowahi kuchezea miaka ya sitini kama vile timu ya shele ya Sekondari ya Mzumbe, timu ya mkoa wa Morogoro, timu ya Polisi na badaye aliwahi kuichezea Simba akiwa na akina Hamisi Kilomoni” alisema Taalib.
Alisema sherehe hizo pia zitapambwa na wasani kutoka vikundi mbalimbali vya ngoma na sarakasi kutoka jijini Dar es Salaam na mkoa wa Pwani..
Alisema SHIWATA ilimzawadia uanachama wa heshima mchezaji huyio baada ya kuchaguliwa kuwa mchezaji bora wa Afrika na kutangaza kumpatia eneo la ekari tano kwa ajili ya kujenga kituo cha wanamichezo
No comments:
Post a Comment