Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Elias Kwandikwa (kushoto) akizungumza katika kikao cha kubadilishana uzoefu kati ya wajumbe wa nchi ya Lesotho na Tanzania. Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi wa Lesotho, Mhe. Lehlohonolo Moramotse (kulia) ameongoza ujumbe huo uliokuja kwa ziara ya mafunzo nchini Tanzania.
Baadhi ya maofisa waandamizi kutoka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano nchini wakiwa kwenye kikao cha kubadilishana uzoefu kati ya wajumbe wa nchi ya Lesotho na Tanzania.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), Eng. Patrick Mfugale akielezea namna TANROADS inavyotekeleza kazi zake kwenye kikao cha kubadilishana uzoefu na wajumbe wa nchi ya Lesotho na Tanzania. Ujumbe huo unaongozwa na Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi wa Lesotho, Mhe. Lehlohonolo Moramotse pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi wa Lesotho, Mathabathe Hlalele.
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano nchini Eng. Joseph Nyamhanga (kulia) akisalimiana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi wa Lesotho, Mathabathe Hlalele (kushoto) mara baada ya kuwasili katika ofisi za Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano za jijini Dar es Salaam katika ziara ya mafunzo. Katikati ni Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi wa Lesotho, Mhe. Lehlohonolo Moramotse.
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi wa nchi ya Lesotho, Mathabathe Hlalele (katikati) akizungumza kwenye kikao cha kubadilishana uzoefu kati ya wajumbe wa nchi hiyo na Tanzania.
Baadhi ya maofisa waandamizi kutoka Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi nchini Lesotho wakiwa katika kikao cha kubadilishana uzoefu kati ya wajumbe wa nchi hiyo na Tanzania.
Kikao cha wajumbe hao katika ofisi za Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) kikiendelea
Baadhi ya maofisa watendaji wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) wakieleza namna ya utekelezaji miradi mbalimbali iliyo chini ya wakala hiyo.
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi wa Lesotho, Mhe. Lehlohonolo Moramotse (kulia) akizungumza katika kikao cha kubadilishana uzoefu kati ya wajumbe wa nchi ya Lesotho na Tanzania. Kushoto ni Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Elias Kwandikwa akiwa katika mazungumzo hayo.
No comments:
Post a Comment