Mshindi wa shindano la Big Brother Africa mwaka 2014 Idris Sultan amesema kwa sasa anafurahia sana kazi mpya ya utangazaji aliyopata katika kituo cha Radio cha Choice FM kilicho chini ya management moja na kile cha Clouds FM..
WALIMU wa shule ya msingi Kianda wameanza mgomo wa siku mbili wa kutofundisha shuleni hapo huku wakilaani kitendo cha Ofisa Elimu (Shule za Msingi) wa Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga mkoani Rukwa, Peter Fusi kumshambulia na kumpiga makofi mwalimu mwenzao akiwa darasani mbele ya wanafunzi wake.
Ikiwa zimepita siku kadhaa toka msanii Shilole afunguke kwenye kipindi cha 5Selekt kinachorushwa kwenye ting'a namba moja kwa vijana EATV kuwa hakuna msanii wa bongo fleva mzuri zaidi yake, mashabiki wameamua kutoa ya mioyoni.