Watu wawili wanaodaiwa kuwa majambazi wameuawa kwa kupigwa risasi na polisi mkoani Mwanza baada ya kurushiana risasi na askari wakati wakiwa kwenye harakati za za kuvamia nyumbani kwa mfanyabiashara wa madini, Baraka Said.
Ni ukumbi wa ndani kwa ndani maarufu mno jijini New York, Marekani nyumbani kwa wasanii wakubwa wakiwemo Jay Z, Beyonce, Justin Bieber, Rihanna, Drake, taja kila msanii mkubwa wa Marekani, amewahi kutumbuiza hapo.
Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Mbeya Mjini, Saadati Mwambungu pamoja na wajumbe 19 wa kamati ya utendaji wa wilaya hiyo, wamevuliwa uongozi baada ya kutuhumiwa kukihujumu chama.
Sakata la kuhamishwa kwa wafanyabiashara wadogo katikati ya Jiji la Dar es Salaam limeingia mdudu baada ya madiwani wa Ukawa kugomea uamuzi uliotolewa na uongozi wa jiji hilo.