Meneja Mawasiliano wa SUMATRA Bw. David Mziray amesema kutokana na majukumu iliyopangiwa SUMATRA inajikita sana kusimamia vyombo vya usafiri binafsi zaidi na vyombo vinavyofanya biashara ya abiria mizigo.
Mziray ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na East Africa Drive kuhusu adha wanayokumbana nayo abiria wanaotumia vivuko vinavyovusha watu kwenda Kigamboni.
''Hivi vivuko vinavyo fanya usafiri wa kuvusha watu kigamboni ni vya serikali kupitia TEMESA ndiyo maana sisi tunakuwa tumewekewa kikwazo kwa mujibu wa sheria kuweza kuvisimamia katika ubora na idadi ya abiria ila sisi huwa tunatoa ushauri pale tunapoona kua dalili ya kutokuwa na usalama kuna wakati tuliwaandikia MV Magogoni wasipakie malori hadi walipofanya matengenezo''-Amesema Mziray.
Aidha Mziray amesema kwa sasa wanajiandaa kufanya marekebisho ya sheria ili kuipa SUMATRA iruhusiwe kuvikagua na kutoa maamuzi ya vyombo hivyo ili kuepuka ajali. |
No comments:
Post a Comment