Thursday, 5 May 2016

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Ijumaa ya May 6.

Dilma Rousseff alia na msemaji bungeni.


Mahakama kuu nchini Brazil imemsimamisha msemaji mwenye nguvu kutoka kwenye bunge la nchi hiyo baada ya kutuhumiwa na Rais Dilma Rousseff kuwa anachochea kesi pamoja na mashtaka yanayomkabili.

Umoja wa Ulaya ilinde mipaka.

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amewataka viongozi wa Ulaya kulinda mipaka ya nje ya umoja wa Ulaya ama kukiwa na hatari kila nchi itapaswa kujilinda yenyewe.

Nigeria bado yashambuliwa na jeshi kisa kipo Hapa.

Maafisa usalama nchini Nigeria wamesema wanamgambo wameshambulia mkondo wa mafuta katika jimbo la Delta.wanaripotiwa kuharibu vibaya mitambo na vifaa

Rihanna na Drake wamekuwa kwenye mahusiano ya siri kwa zaidi ya mwezi 1 sasa.

Jarida la PEOPLE limefumua bonge moja la siri kuwa staa Rihanna na rapa Drake wamekuwa na mahusiano ya siri kwa zaidi ya mwezi mmoja sasa.