Mahakama kuu nchini Brazil imemsimamisha msemaji mwenye nguvu kutoka kwenye bunge la nchi hiyo baada ya kutuhumiwa na Rais Dilma Rousseff kuwa anachochea kesi pamoja na mashtaka yanayomkabili.
Hakimu wa mahakama hiyo amesema kuwa msemaji huyo Eduardo Cunha,hakupaswa kuongoza mkutano wowote kwavile anashutumiwa kwa kuhusika katika rushwa kwa namna nyingi.
Waendesha mashtaka wanamshutumu kwa kuchukua mamilioni ya dola kama rushwa huku akitumia nafasi yake kuzuia uchunguzi kuhusu rushwa ya kampuni ya mafuta ya Petrobras.
Kama mahakama kuu haitatengua uamuzi huo,kusimamishwa kwa Cunha kutakuwa kwa muda mrefu.
No comments:
Post a Comment