Timu ya Manchester City imeshindwa kutinga fainali za Ligi ya Mabingwa Ulaya katika mchezo mkali wa pili wa nusu fainali dhidi ya timu ya Real Madrid nchini Hispania.
Baada ya kutoka sare tasa katika mchezo wa awali, Real Madrid walipata goli pekee katika mchezo huo kupitia krosi ya Gareth Bale iliyogongwa na Fernando na kujikuta akijifunga.
Mpira wa Fernandinho uligonga mwamba katika moja ya nafasi chache za Manchester City, lakini Real Madrid ilitawala huku shuti la Bale likigonga mwamba na Kipa Joe Hart akiokoa michomo ya Luka Modric na Cristiano Ronaldo.
Gareth Bale akipiga krosi iliyogongwa na Fernando na kuingia wavuni
Kipa Joe Hart akishindwa kuuzuia mpira uliogongwa na Fernando na kutinga wavuni
No comments:
Post a Comment