PITOMA NEWS ONLINE.BLOGSPOT.COM
WAZIRI Mkuu mteule wa Serikali ya Awamu ya Tano, Kassim Majaliwa, amewaahidi raha wanamichezo, akisema ni eneo analolifahamu vyema na wasihofu katika hilo. Kutokana na hali hiyo amesema atamshauri Rais John Magufuli kumteua Waziri atakayeshughulikia michezo yule ambaye ana uelewa mpana zaidi wa mambo ya michezo.
“Mimi ni kocha mwenye leseni ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF), ni mkufunzi wa TFF (Shirikisho la Soka Tanzania), ni kocha niliyesomea hasa na pia kuifanya hiyo kazi. “Najua wanamichezo wanahitaji mambo gani, naelewa sasa michezo ni ajira pia ni afya, hilo ni eneo langu.
“Nataka kupitia michezo tujitangaze, wanamichezo wawe mabalozi wetu wazuri, wasihofu mwanamichezo mwenzao nipo,” alisema Waziri Mkuu mteule huyo na kuongeza kuwa hata jana asubuhi alikuwa Uwanja wa Jamhuri, Dodoma kufanya tishwa na Bunge jana kuwa Waziri Mkuu wa 11 wa Tanzania.
Waziri Mkuu huyo ambaye anatarajiwa kuapishwa leo mjini hapa, alipata kura za ndiyo 258 sawa na asilimia 73.5, ushindi ulioelezwa na Spika wa Bunge, Job Ndugai kwamba ni wa kishindo.
Akisoma matokeo ya upigaji kura za kumthibitisha, Katibu wa Bunge, ambaye alikuwa msimamizi wa uchaguzi huo, Dk Thomas Kashililah, alisema kura zilizomkataa zilikuwa 91, sawa na asilimia 25.9.
Kwa mujibu wa Dk Kashililah, kura zilizopigwa zilikuwa 351 na kura mbili ziliharibika, ambapo wabunge waliosajiliwa kwa ajili ya Bunge hilo ni 369. Idadi ya wabunge kikatiba ni 394.
Licha ya kuwa Kocha Mkuu wa Bunge SC, Majaliwa amepata kuwa kocha wa timu mbalimbali mkoani Mtwara, pia amekuwa mkufunzi wa michezo na alikuwa kocha wa timu mbalimbali katika mashindano ya shule za msingi (Umitashumta) na sekondari (Umisseta) miaka ya nyuma.
Majaliwa anakuwa Waziri Mkuu wa 11, waliomtangulia wakiwa Mwalimu Julius Nyerere, Rashidi Kawawa, Edward Sokoine (wote marehemu), Cleopa Msuya, Dk Salim Ahmed Salim, Joseph Warioba, Dk John Malecela, Frederick Sumaye, Edward Lowassa na Mizengo Pinda.
Mbunge wa Nzega Vijijini, Dk Hamisi Kigwangwala alisifu uteuzi huo na kwamba ni furaha kubwa kwa wanamichezo kwani Majaliwa ni mwanamichezo hasa na anayeijua vyema michezo. Hata hivyo, Kigwangwala alieleza hofu yake kama ataendelea kupata fursa ya kufanya mazoezi na wabunge na pia ataendelea kuwa kocha wa timu ya Bunge SC.
Mbunge wa Kilolo, ambaye pia ni mchezaji wa zamani wa mpira wa miguu katika timu mbalimbali na timu ya Taifa ‘Taifa Stars’, Venance Mwamoto, alisifu uteuzi wa Waziri Mkuu mwanamichezo.
“Huyu ni mwanamichezo halisi, sio tu kuipenda bali pia kucheza, tunamuahidi ushirikiano mkubwa sisi wanamichezo,” alisema Mwamoto na kumpongeza Rais wa Tanzania, Dk John Magufuli kwa uteuzi huo. Majaliwa aliyekuwa Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa akishughulikia elimu katika Serikali ya Awamu ya Nne, alithibiti.
No comments:
Post a Comment