Mdhibiti
na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Juma Assad
akionesha ripoti ya ukaguzi ya mwaka wa fedha unaoishia Juni 30, 2015
kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) leo mjini Dodoma ili iweze
kujadiliwa na wabunge katika Bunge la bajeti ya mwaka 2016/2017.
Mdhibiti
na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Juma Assad
akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo mjini Dodoma juu ya
ripoti ya ukaguzi ya mwaka wa fedha unaoishia Juni 30, 2015 ili iweze
kujadiliwa na wabunge katika Bunge la bajeti ya mwaka 2016/2017.
Waandishi
wa habari wakipokea ripoti ya ukaguzi ya mwaka wa fedha unaoishia Juni
30, 2015 ili iweze kujadiliwa na wabunge katika Bunge la bajeti ya mwaka
2016/2017.
Mdhibiti
na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Juma Assad
amekabidhi ripoti ya ukaguzi ya mwaka wa fedha unaoishia Juni 30, 2015
bungeni leo ili iweze kujadiliwa na wabunge katika Bunge la bajeti ya
mwaka 2016/2017.
Katika
ripoti yake, CAG ametoa mapendekezo kadhaa ambayo yanatakiwa kufanyiwa
kazi ili kuboresha matumizi ya fedha za Serikali kwa malengo
yanayokusudiwa.
Miongoni
mwa maeneo ambayo CAG ametoa mapendeklezo ni Ofisi ya Masjili wa Vyama
vya Siasa nchini ifuatilie suala la uwasilishaji wa taarifa za fedha kwa
wakati kulingana na matakwa ya sheria.
Hatua
hiyo ya CAG inafuatia ukaguzi uliofanywa kwenye vyama vya siasa nchini
vyenye usajili wa kudumu ambavyo jumla yao ni vyama 22.
Prof.
Assad alisema kuwa kati ya vyama hivyo vyenye usajili wa kudumu, ni
chama kimoja ndicho kilichowasilisha hesabu zake kwa kipindi cha miezi
sita kuanzia Januari hadi Juni 2015 ambacho ni Chama cha Wananchi (CUF).
Vyama
vingine 21 havikuwasilisha vitabu vya hesabu kwa ajili ya ukaguzi
kinyume cha kifungu Na. 14 cha Sheria ya vyama vya siasa Na. 5 ya mwaka
1992.
No comments:
Post a Comment