Meneja wa Diamond Platnumz ‘Bab Tale’ ambaye hivi karibuni amejitoa
kumsaidia rapa Chid Benz kuacha matumizi ya dawa za kulevya ameongelea
mara ya kwanza kuona picha za Chid Benzi akiwa kwenye hali aliyopo kwa
sasa.
Kupitia #PlanetBongo Babutale amesema “Kusema
ukweli nilipoona picha ile nilipata wasiwasi nikidhani Chid Benzi labda
ameungua na maradhi yetu ya sasa, sikuamini kama ni madawa ya kulevya
ndiyo yamempelekea hali ile,lakini sikuweza kuamini kesho yake ilibidi
nimchukue Chid Benzi na kwenda nae kwenye kituo cha afya na kufanya
check up ya mwili mzima, lakini baada ya vipimo kutoka akaonekana yuko
poa kabisa ila wakagundua tu ni hayo madawa” alisema Chid Benzi.
Katika hatua nyingine Babu tale amesema yeye ameamua kumsaidia Chid
Benzi ili aweze kurudia katika hali yake ya kawaida na aendelee na
maisha yake ya kawaida na si kusema ameamua kumsaidia kwa sababu ya
kutafuta kiki au kutafuta maslahi kama ambavyo baadhi ya watu wamekuwa
wakidai. |
No comments:
Post a Comment